https://tpc.googlesyndication.com/simgad/8045142562622600543


Recent Post

Saturday, April 19, 2014

Yanga chupuchupu kuchezea kichapo kutoka kwa Simba, Azam washinda tena


Timu ya Yanga leo imeshindwa kujibu kipigo cha mtani wake wa jadi, Simba, baada ya kutoka sare ya bao 1-1, mechi iliyopigwa katika Uwanja wa Taifa, jijini Dar es Salaam.

Bao la Simba lilipatikana katika dakika ya 75 kupitia kwa Haruna Chanongo wakati lile la Yanga liliingia dakika ya 88 kupitia kwa Simon Msuva, katika mechi iliyokuwa na vituko vya aina yake.


Katika mechi hiyo iliyokuwa na msisimko wa aina yake, mlinda mlango wa Simba, Ivo Mapunda, hatashindwa kuisahau baada ya taulo lake kuibua kizaa zaa na kulazimika kutupwa nje na wachezaji wa Yanga, wakiongozwa na Khamis Kiiza.


Katika mechi hiyo, Yanga ndio waliokuwa na shauku ya kushinda kutokana na kushika nafasi ya pili katika msimamo wa Ligi, huku ikiwa na kumbukumbu ya kupigwa bao 3-1 katika mechi ya mtani jembe iliyowaacha mashabiki wake njia panda.


Awali mpira ulianza kwa kasi huku kila timu ikijipanga kushinda katika dakika za mwanzo za mchezo huo.  Timu ya Simba iliweza kumiliki vyema dakika tano za kwanza, kabla ya Yanga kuzinduka na kujibu mashambulizi ya mtani wake.


Katika mechi nyingine, timu ya Azam iliibuna na ushindi wa bao 1-0 dhidi ya JKT Ruvu, mechi iliyopigwa katika Uwanja wa Chamazi, jijini Dar es Salaam, hivyo kumaliza bila kufungwa sambamba na kufanikiwa kutwaa ubingwa wa Bara, huku bao la pekee likipatikana katika dakika ya 79 kupitia kwa Brian Umony.


Mkoani Tanga, timu ya Kagera Sugar iliweza kuibuka na ushindi wa bao 1-0 dhidi ya Coastal Union ya mkoani humo, huku bao lao likipatikana   

dakika ya 50 kupitia kwa Themi Felix, akitumia kazi nzuri ya Paul Ngwai.




UKAWA watoa ukweli wa habari za kumbembeleza Zitto Kabwe, walia mikutano yao Zanzibar kupigwa marufuku

Baadhi ya Watanzania Visiwani Zanzibar wakionyesha ishara ya kuhitaji serikali tatu leo mjini Zanzibar ikiwa ni siku moja baada ya serikali kupitia jeshi la Polisi kupiga marufuku mikutano ya Umoja wa Katiba ya Wananchi (UKAWA). Yafuatayo ni maandishi ya Julius Mtatiro, Naibu Katibu Mkuu BARA wa CUF, ambaye pia ni Mjumbe wa Baraza la Katiba aliyesusa na wenzake.....

CCM WASIONESHE UDHAIFU KWA PROPAGANDA ZA KITOTO NAMNA HII;

Habari inayoenezwa kuwa viongozi wakuu wa UKAWA na hata waandamizi nikiwemo mimi, eti tumembembeleza mhe. Zitto Kabwe ili aunge mkono mikutano ya UKAWA kuzunguka nchi siyo taarifa zenye ukweli wowote.

Mhe Zitto hajawahi kufuatwa na viongozi kuombwa ashiriki ktk shughuli za UKAWA. Na hadi sasa UKAWA haijatangaza shuguli zozote zile zaidi ya mkutano wa Zanzibar ambao pia polisi wamekataa usifanyike leo hadi mara nyingine.

Kwa bahati nzuri, wakati mhe. Zitto Z Kabwe akichangia sura ya 1 na ya 6 bungeni, alionesha njia sahihi kwa taifa na kwa asilimia mia moja aliunga mkono hoja za wananchi na hata mapendekezo ya UKAWA.....Kwa mfano Zitto Kabwe alisema, "hoja ya serikali tatu kuvunja muungano siyo ya kweli. Alisisitiza kuwa muungano unaweza kuvunjika ndani ya serikali moja, mbili, tatu na hata tano"

Ujumbe wa UKAWA ni HIYARI. Ndiyo maana baadhi ya wajumbe kama ISACK CHEYO wali-walk out pamoja na UKAWA bungeni lakini keshoye walirejea na kuendelea na bunge.

Umoja huu unaheshimu haki wajibu na maamuzi ya kila mtu. Msimamo wa UKAWA ni kulinda na kutetea rasimu ya maoni iliyoletwa na tume ya mabadiliko ya katiba kwa msingi wa kulinda mamlaka na maoni ya wananchi.

Tutafanya kazi na mtu yeyote ambaye anaamini yale tunayoyasimamia. Hatutamuomba mtu yeyote asiyeona uzito wa hoja zetu atuunge mkono, badala yake tutaendelea kuwaheshimu wote wanaotofautiana nasi kwa hoja huku tukiendelea kupigania kile ambacho tunakiamini.

J. Mtatiro,
UMOJA WA KATIBA YA WANANCHI(UKAWA),
Zanzibar.

Soka la ufukweni kuanza kutimua vumbi kesho



Na Mwandishi Wetu, Dar es Salaam
MICHUANO ya mpira wa miguu ya ufukweni (Beach Soccer) inazinduliwa rasmi kesho (Aprili 20 mwaka huu) kwenye ufukwe wa Escape One uliopo Mikocheni, Dar es Salaam na kushirikisha timu 13.

Uzinduzi huo utaanza saa 5 asubuhi na mechi zitachezwa hadi saa 11 jioni. Michuano hiyo inayofanyika kwa mara ya kwanza nchini inashirikisha timu 13 kutoka vyuo mbalimbali vya jijini Dar es Salaam.

Vyuo hivyo ni Chuo Kikuu cha Ardhi (AU), Chuo Kikuu cha St. Joseph Tanzania (SJUIT), Chuo Kikuu cha Tumaini Dar es Salaam (TUDARCO), Chuo cha Ustawi wa Jamii (ISW), Chuo cha Uandishi wa Habari Dar es Salaam (DSJ) na Chuo cha Kumbukumbu ya Mwalimu Nyerere.

Vingine ni Chuo cha Utumishi wa Umma Magogoni, Chuo cha Usimamizi wa Fedha (IFM), Chuo cha Elimu ya Biashara (CBE), Taasisi ya Teknolojia Dar es Salaam (DIT), Taasisi ya Uhasibu Tanzania (TIA), Chuo cha Utawala wa Kodi (ITA) na Chuo cha Taifa cha Usafirishaji (NIT).

Michuano hiyo itakuwa inachezwa Jumamosi na Jumapili kwenye fukwe za Escape One na Gorilla Beach iliyopo Kigamboni, Dar es Salaam.

23 waitwa kuungana na nyota 16 wa Taifa Stars



Na Kambi Mbwana, Dar es Salaam
KOCHA Msaidizi wa Taifa Stars, Salum Mayanga ametangaza wachezaji wengine 23 watakaoingia kambini kesho (Aprili 20 mwaka huu) kuungana na 16 waliotajwa awali kujiandaa kwa mechi ya kirafiki dhidi ya Burundi itakayochezwa Aprili 26 mwaka huu.

Wachezaji walioitwa ni makipa Aishi Manula (Azam), Deogratias Munishi (Yanga) na Mwadili Ali (Azam). Mabeki ni Abdi Banda (Coastal Union), Aidan Michael (Ruvu Shooting), Aggrey Morris (Azam), Erasto Nyoni (Azam), Hassan Mwasapili (Mbeya City), Kelvin Yondani na Said Moradi (Azam).

Viungo ni Amri Kiemba (Simba), Frank Domayo (Yanga), Himid Mao (Azam) na Jonas Mkude (Simba).

Washambuliaji ni Athanas Mdamu (Alliance), Haruna Chanongo (Simba), Juma Liuzio (Mtibwa Sugar), Khamis Mcha (Azam), Mbwana Samata (TP Mazembe, DRC), Mrisho Ngasa (Yanga), Mwinyi Kazimoto (Markhiya, Qatar), Ramadhan Singano (Simba), Simon Msuva (Yanga) na Thomas Ulimwengu (TP Mazembe, DRC).

Wachezaji walioitwa kutoka katika kikosi cha maboresho ni kipa Benedicto Tinoko Mlekwa (Mara), mabeki wa kati; Emma Namwondo Simwanda (Temeke) na Joram Nason Mgeveje (Iringa). Walinzi wa pembeni ni Omari Ally Kindamba (Temeke), Edward Peter Mayunga (Kaskazini Pemba) na Shiraz Abdallah Sozigwa (Ilala).

Viungo ni Yusuf Suleiman Mlipili (Temeke), Said Juma Ally (Mjini Magharibi), Abubakar Ally Mohamed (Kusini Unguja), Hashim Ramadhan Magona (Shinyanga), Omari Athumani Nyenje (Mtwara) na Chunga Said Zito (Manyara).

Washambuliaji ni Mohammed Seif Saidi (Kusini Pemba), Ayoub Kasim Lipati (Ilala), Abdurahman Othman Ally (Mjini Magharibi), Paul Michael Bundara (Ilala). Wachezaji wa U 20 ni Mbwana Mshindo Musa (Tanga) na Bayaga Athanas Fabian (Mbeya).

Taifa Stars inayodhaminiwa na Kilimanjaro Premium Lager itaingia kambini kwenye hoteli ya Kunduchi Beach.

Thursday, April 17, 2014

Chadema, CUF na TLP kuanza ziara za mikoani kuishtaki CCM kwa wananchi



Na Mwandishi Wetu, Dar es Salaam
MUUNGANIKO wa vyama vya upinzani, Chadema, CUF na TLP wamepanga kuanza kufanya mikutano ya kuelimisha wananchi juu ya mambo mbalimbali, ikiwamo Katiba Mpya. Muunganiko huo uliopewa jina la UKAWA, utaanza kufanya mikutano yao Visiwani Zanzibar kuanzia Jumamosi.

Baadhi ya wajumbe wa UKAWA wakijadiliana jambo Bungeni Dodoma. Wajumbe hawa walisusa na kutoka nje ya Bunge jana mjini Dodoma.
Mtu wa karibu na mdau wa mambo ya kisiasa na mwelekeo wa Katiba Mpya, aliudokeza mtandao huu kuwa dhamira ya UKAWA kufanya mikutano katika Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ni kuishtaki serikali ya CCM kwa wananchi, kwa madai wanataka kupora haki ya Katiba.

Mikutano hiyo itaanza kufanyika siku chache baada ya UKAWA kususa Bunge la Katiba linaloendelea mjini Dodoma; jambo ambalo limeibua hisia tofauti kwa Watanzania.

“Hawa jamaa wanataka kuzunguuka katika mikoa ya Tanzania Bara, wakianzia na Zanzibar Jumamosi kwa ajili kuishtaki serikali ya CCM kwa madai kuwa inataka kuandika Katiba ya CCM badala ya Watanzania wote,” alisema.

Taarifa zaidi za mikutano ya UKAWA katika maeneo mbalimbali ya Tanzania zitaendelea kukujia hatua kwa hatua.

Mabadiliko ya elekeo wa barabara katikati ya jiji la Dar es Salaam

MABADILIKO YA UELEKEO WA BARABARA KATIKATI YA JIJI LA DAR ES SALAAM KUANZIA SIKU YA JUMATATU TAREHE 28/04/2014. CHANGE OF TRAFFIC CIRCULATION AT THE CBD WITH EFFECT FROM MONDAY 28th APRIL 2014
Ramani ya barabara jijini Dar es Salaam. Picha kwa hisani ya wadau wa barabara.
1. Kipande cha Mtaa wa Samora kuanzia Mnara wa Askari (Askari Monument) hadi Clock Tower Magari kutakuwa na mabadiliko ambayo magari yatakuwa yanaelekea Clock Tower badala ya Askari Monument.
2. Barabara ya Sokoine kuanzia Station hadi Makutano ya Mtaa wa Maktaba Posta Ya Zamani Magari yatakuwa yanaelekea Uelekeo mmoja wa Station Posta ya Zamani tofauti na ilivyo sasa Posta ya Zamani kwenda Station.
3. Barabara ya Kivukoni Kuanzia Posta ya Zamani hadi Ferry itakuwa barabara ya mielekeo miwili (Two Ways).
4. Barabara ya Samora kuanzia Mnara wa Askari hadi Ocean Road Hospitali itakuwa ni barabara ya mielekeo miwili.
5. Daladala Zote zitakazotokea barabara za Makataba zitakunja kulia pembeni ya Jengo la NBC na hadi Makutano ya Mkwepu na kukunja kushito kuingia Sokoine pale Posta ya Zamani na baadaye kukunja kushoto kuingia Makataba na kurudi Posta Mpya .
Key:
1. RANGI YA NJANO - Njia ya Uelekeo Mmoja {One Way}.

2. RANGI YA BLUE MPAUKO - Njia ya Mielekeo Miwili {Two Way}
3. RANGI YA KIJANI - Mitaa ya Kutembea kwa Miguu Magari marufuku {Walking Streets}
4. RANGI NYEKUNDU - Barabara za kupita Daladala
5. RANGI YA BLUU ILIYOIVA - Barabara za DART
6. DUARA ZA NJANO - Mzunguuko {Roundabout}
7. MSALABA WA KIJANI - Makutano yenye Taa za kuongozea Magari {Singnalized Intersection}
Kwa Maelezo zaidi Wasiliana na Ofisi za DART
UBUNGO PLAZA GHOROFA YA KWANZA.

AU.
OFISI YA MHANDISI WA MANISPAA YA ILALA
MABALA NA SHOPRITE SUPEEMARKET JIRANK NA KAMATA

Mtaarifu mwingine juu ya mabadiliko haya kuondoa usumbufu ifikapo siku ya Jumatatu 28/04/2014. PASAKA NJEMA

Simba waipania vilivyo Yanga SC



Na Mwandishi Wetu, Dar es Salaam
KATIBU Mkuu wa Simba, Ezekiel Kamwaga, amesema kwamba wana kila sababu ya kushinda katika mechi yao dhidi ya Yanga Jumamosi ili waweke heshima kwa soka la Tanzania.
Simba jana iliondoka na kuelekea Visiwani Zanzibar walipoweka kambi yao kwa ajili ya kujiwinda na mechi ya mtani wao wa jadi, Yanga itakayopigwa Jumamosi katika Uwanja wa Taifa, jijini Dar es Salaam.
Akizungumza leo mchana, Katibu Mkuu Kamwaga alisema kuwa hawana wasiwasi na mechi yao na Yanga, wakiamini kuwa watajenga heshima yao kwa soka la Tanzania.
Alisema wanaamini kwa pamoja wachezaji wote watafanya kazi nzuri kujiandaa kwa ajili ya mchezo huo muhimu unaosubiriwa kwa hamu na wadau wa soka hapa nchini.
“Tunajiamini kuwa matokeo mazuri ya uwanjani yatatuweka katika nafasi nzuri kushinda mbele ya Yanga, ukizingatia kuwa timu ipo vizuri na imejiweka sawa Visiwani Zanzibar.
Benchi la ufundi kwa pamoja linajua namna gani tuna kila sababu ya kushinda mbele ya Yanga, ukizingatia kuwa timu yetu imepata nafasi mbaya kiasi cha kushindwa kutwaa ubingwa wa Bara,” alisema.
Mbali na kushindwa kutwaa ubingwa wa Bara, Simba pia imeshindwa walau kushika nafasi ya pili, ikiambulia nafasi ya nne kwa kujikusanyia pointi 37 katika ligi.

Picha mbalimbali za ziara ya Kinana Mkoani Katavi

 Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana na ujumbe wake wakipata maelezo kutoka kwa Daktari wa Kituo cha Afya Inyonga Dk. Koni, Katibu Mkuu alitembelea kituo hicho ambacho kimeombewa kibali cha kuwa Hospitali ya wilaya tangia mwaka jana mwezi Februari lakini mpaka sasa maombi hayajajibiwa wala mkaguzi kutoka Wizara ya Afya hajafika kituoni hapo, kituo hicho ni kikubwa chenye vitanda 90 na uwezo wa kulaza wagonjwa 60 kwa mara moja, kina majengo ya kutosha na vifaa vya kutosha kuwa Hospitali ya wilaya.
 Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akiangalia baadhi ya vifaa vipya kabisa vya kituo hicho cha afya cha Inyonga wilayani Mlele ambacho kinaomba kupatiwa hadhi ya kuwa hospitali ya Wilaya .

LinkWithin

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...