Na Luteni Selemani Semunyu JWTZ
Wachezaji Watatu wa Timu ya Golf ya Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania ya Lugalo wameteuliwa kujiunga na timu ya Taifa ya mchezo huo ikiwa ni mara ya kwanza tangu kuanzishwa klabu hiyo miaka 10 iliyopita kupata idadi hiyo.
Akiongea na mwandishi wa habari hizi Jijini Dar es Salaam nahodha wa Klabu hiyo ya Lugalo Kapteni Japhet Masai alisema hatua hiyo ya furaha kwa klabu yao imekuja baada ya mashindano ya wazi ya Arusha Open yaliyomalizika hivi karibuni Jijini Arusha.
Mchezaji wa Golf wa Klabu ya Jeshi ya Lugalo Michael Obare
ambaye ameteuliwa kujiunga na Timu ya taifa akiwa kwenye harakati za Mcheo huo
hivi karibuni Jijini Arusha. Picha na Luteni
Selemani Semunyu.
”Ni mara ya kwanza na imekuja Muda Mchache baada ya klabu kupata Mwenyekiti mpya Brigedia Jenerali Michael Luwongo pengine ni ishara njema ya Uongozi wake katika klabu hiyo yenye malengo makubwa ya kubor eshwa.” Alisema Masai.
Aliongeza kuwa Klabu hiyo iliwahi kutoa Mchezaji Mmoka Mwaka 2012 sasa hii ni kwa mara ya kwanza kwa Klabu hiyo kutoa Wachezaji wa Timu ya Taifa zaidi ya mmoja tangu kuanzishwa kwa klabu hiyo Miaka 10 iliyopita na kutoa mchezaji hata mmoja Tangu Mwaka 2012.
Aliwataja wachezaji hao kutoka Lugalo ni Michael Obare ,Richard Mtweve na Henrick Nyenza ambao wataungana na wachezaji wengine 11 katika mchujo utakaofanyika katika Viwanja vya Klabu ya Lugalo Jumamosi Oktoba 22 ili kupata wachezaji 10 kati yao akiwemo mmoja wa Akiba.
Aliongeza kuwa sasa wachezaji hao wanajiandaa na mchujo ili jumamosi chini ya Uangalizi wa Wachezaji wa kulipwa waweze kufanya vizuri na wajumuishwe katika kikosi huku Wachezaji watalazimika kucheza Mikwaju ya Jumla Gross 74.
Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa hivi karibuni na Mwenyekiti wa chama cha Golf Tanzania Joseph Tango aliwatangaza wachezaji wengine walioitwa kuwa ni Isack Wanyenche (Kili Golf), Abbas Adam (Moshi Club),Adam Said (Moshi Club).
Wengine walioitwa ni Elisha Mbwambo (TPC),George Sembi(TPC),Victor Joseph (Dar Gymkhana),Amani Said (Dar Gymk(Dar Gymkhana),Salim Shariff (Dar Gymkhana),Idan Iziku (Dar Gymkhana) ,Jay Nathwani (Gymkhana Arusha),Pravin Singh(Gymkhana Arusha).
Kwa Mujibu wa taarifa hiyo wachezaji hao wanatarajia kuwakilisha Nchi katika mashindano ya Afrika Mashariki East Afrika Golf Challenge Edition 2016 nchini Ethiopia na wanatarajiwa kuanza kambi Jijini Dar es Salaam.
No comments:
Post a Comment