Waumini wa Kanisa Katoliki wakiandamana wakati wa kuanza ibada ya Masista wa Jimbo la Dar es Salaam wa Shirika la Dada Wadogo la Mbagala Misheni baada ya kutembelewa na Umoja wa Wanaume wa Kanisa Katoliki (Uwaka), Dar es Salaam leo asubuhi, ambao jukumu lao kubwa ni kuwalea watawa hao.
Na Dotto Mwaibale
WATANZANIA wametakiwa kuacha tabia ya kuchagua kazi na kudharau kazi zingine kwani mbele za mungu kazi zote ni sawa na zinaheshimika.
Hayo yameelezwa na Monsinyori Padri Deogratius Mbiku katika ibada takatifu ya kuombea Umoja wa Wanaume Katoliki (Uwaka) kuwasaidia kwa hali na mali masista wa Shirika la Dada Wadogo wanaoishi eneo la Mbagala Misheni jijini, Dares Salaam.
Akitoa mahubiri katika ibada hiyo, alisema binadamu anapenda kuchagua kazi huku akionya kuwa watu waache kudharau kazi yoyote inayofanywa na mwingine ilimradi iwe ya halali.
Monsinyori Padri Deogratius Mbiku . wa Parokia ya Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM) (katikati), akiongoza ibada ya misa takatifu. Kushoto ni Padri Msaidizi wa Kanisa la Katoliki la Mtakatifu Joseph, Edward Sabbas na kulia ni Katibu wa Jimbo hilo, Aidan Mubezi.
Askofu Mkuu wa Kanisa Katoliki Jimbo Kuu la Dar es Salaam, Mwadhama Polycarp Kardinali Pengo (kulia), akishiriki sakramenti takatifu wakati wa ibada hiyo. |
Baadhi ya waumini wa kanisa hilo wakinunua mvinyo wa Arovela.
Waumini wakisali mbele ya msalaba nje ya kibanda maalumu cha msalaba wa Yesu.
Mapadri na watumishi wa kanisa wakitoka kwenye ibada hiyo.
“Tusidharau tufanye kazi na asiye fanya kazi hastahili kula. Hata familia yaYesu ililala njaa…hata ukilala njaa usidharau kazi,”alisema.
Akimzungumzia Hayati Baba wa Taifa Mwalimu Nyerere, PadriMbiku alisemaalikuwa mtu wa kwanza kuwaomba masista kuombea nchi ilipovamiwa na majeshi yaIdd Amin wa Uganda.
“Nyerere aliwashukuru sana watawa masista kwa kushinda vita ile dhidi ya Idd Amin. Tanzania haikuzoea vita.
“Hivyo aliomba masista wasali sana. Tanzania ikashinda.
Nyerere alisema waziwazi na washukuru masista kwa kushinda vita,” alisemaMbiku.
Vita kati ya Tanzania na Uganda iliibukamwaka 1978 nakufikia tamati mwaka 1979 baadayamajeshi ya Amin kuchakazwa vibaya na Jeshi la Wananchiwa Tanzania (JWTZ).
Kutokana na umuhimu wa sala za masista hao, Padri Mbiku aliwaomba Uwaka kuhakikisha wanawasaidia masista kwani wanamchango mkubwa kwa taifa na kanisa.
“Masista wanajitoleakuombea kanisa na watu wote wapate wokovu pasipo kubagua dini zao. Sala yao nimuhimu, ina nguvu na Mungu anaisikiliza kwa kujitoa kwao,” alisema.
Kwa msingi huoaliwaomba Uwaka ambao kaulimbiu yao “Nguzo Imara Hekalu la Bwana”
No comments:
Post a Comment