Na Mwandishi Wetu, Dar es Salaam
TAASISI ya kifedha ya Bayport Financial Services inayojihusisha
na mikopo imekabidhi hati za viwanja vya Vikuruti, wilayani Kibaha, mkoani
Pwani kwa baadhi ya wateja waliomaliza kulipa mikopo yao tangu walipochukua
mikopo hiyo yaa viwanja mapema mwaka jana. Baadhi ya wateja waliokabidhiwa hati hizo ni pamoja na
Desidery Didas Kalimwenjuma wa Temeke na James Moses Lubinza wa Kimara jijini
Dar es Salaam, huku hati za wateja wengine zikiwa zimekaamilika kwa ajili ya
kukabidhiwa wateja hao ambao walikuwa miongoni mwa Watanzania waliochangamkia
fursa ya mikopo ya viwanja vya Vikuruti, vilivyokuwa vinauzwa na Bayport kwa
kushirikiana na Kampuni ya Property International Ltd.
Afisa Sheria wa Bayport Financial Services, Mrisho Mohamed (kushoto), akishuhudia bwana James Moses Lubinza akitia sahihi katika tukio la upewaji wa hati yake ya kiwanja cha Vikuruti, Mlandizi, wilayani Kibaha, mkoani Pwani leo mchana, jijini Dar es Salaam. Lubinza alikuwa miongoni mwa Watanzania waliochangamkia fursa ya mikopo ya viwanja vya Bayport. Huduma hizo za viwanja mwaka huu zinaendelea kwa kuanzishwa miradi ya Bagamoyo, Kigaamboni, Chalinze, Kibaha na Kilwa vikuhusisha watumishi wa umma, wafanyakazi wa kampuni binafsi na wajasiriamali. Picha kwa hisani ya Bayport Financial Services.Meneja Masoko na Mawasiliano wa Bayport Financial Services Ngula Cheyo katikati akikabidhi hati ya kiwanja cha Vikuruti kwa mteja wao James Moses Lubinza leo jijini Dar es Salaam. Kushoto ni Afisa Sheria wa Bayport, Mrisho Mohamed.
Akizungumza leo mchana katika makabidhiano hayo jijini Dar es Salaam, Meneja Masoko na Mawasiliano wa Bayport, Ngula Cheyo, alisema ni furaha yao kubwa kuanza kutoa hati ya viwanja vilivyouzwa kwa baadhi ya Watanzania walioamua kuchangamkia fursa za viwanja vyao. Alisema hatua hiyo ni sehemu muafaka ya kuhakikisha kwamba viwanja hivyo vilivyopimwa na vyenye hati vinakuwa sehemu ya kuendeleza na kusaidia wananchi ambao kwa kupitia viwanja hivyo wanaweza kuvitumia katika fursa mbalimbali kama vile mikopo, kujenga nyumba za biashara na makazi ya kuishi wao na familia zao.
Afisa Sheria wa Bayport Financial Services Mrisho Mohamed kushoto akiangalia mteja wao Desidery Didas Kalimwenjuma wakati anatia sahihi katika makabidhiano ya kupewa hati yake ya kiwanja cha Vikuruti, wilayani Kibaha mkoani Pwani.
Afisa Sheria wa Bayport Financial Services Mrisho Mohamed kushoto akimkabidhi hati ya kiwanja cha Vikuruti mteja wao Desidery Didas Kalimwenjuma.
Mwanasheria wa Bayport Financial Services Mrisho Mohamed kushoto akipiga picha ya pamoja na mteja wao Desidery Didas Kalimwenjuma baada ya kumkabidhi hati yake ya kiwanja cha Vikuruti, wilayani Kibaha mkoani Pwani leo mchana.
“Hii ni hatua muhimu kwetu Batyport kuona viwanja vya
Vikuruti vimeanza kutoka kwa hati zao na kuona kila aliyepata kiwanja basi
hatakuwa na usumbufu wowote wa kupewa hati yake, iwe kwenye mradi wa Vikuruti
au maeneo mengine ya Tanzania tunayoendelea na biashara ya kuuza viwanja kwa
njia ya fedha taslimu na mkopo.
“Tunawahakikishia usalama na huduma bora kabisa kutoka kwetu
Bayport, tukiamini kwamba viwanja vyenye hati tunavyotoa ni maeneo mazuri na
yanayoweza kujibu maswali rahisi ya Watanzania wote kuweza kumiliki ardhi kwa
utaratibu rahisi na mzuri,” alisema Cheyo.
Akizungumza baada ya kupewa hati yake, Kalimwenjuma alisema
anashukuru kwa kupata hati yake haraka bila usumbufu wowote, hali inayoonyesha
umakini mkubwa uliokuwapo kwenye huduma hiyo ya mikopo ya viwanja vya Bayport. “Nashukuru kwa sababu nilikuwa miongoni mwa Watanzania
waliojitokeza kununua viwanja vya Bayport na leo nimepigiwa simu kwa ajili ya
kukabidhiwa hati yangu huku nikiwa na furaha kubwa pamoja nja kuwapongeza mno
kwa huduma bora,” Alisema.
Naye Lubinza alisema hajawahi kukutana na huduma bora za
viwanja kama vya Bayport kwa sababu havina longolongo wala usumbufu wowote,
jambo linaloonyesha utulivu na umakini uliozalisha kupewa hati yake haraka bila
tatizo. “Ni maendeleo makubwa kwa kuwekeza fedha zangu kwa kununua
viwanja vya Vikuruti nikiamini kuwa ardhi ni kitu kinachopanda thamani siku
hadi siku, huku nikifurahia zaidi kwa sababu ni miongoni mwa Watanzania
waliopewa hati na Bayport,” Alisema.
Maeneo mengine ya Tanzania ambayo Bayport inatoa mikopo ya
viwanja ni pamoja na Bagamoyo (Kimara Ng’ombe), Kibaha (Boko Timiza), Kilwa
(Msakasa), Kigamboni (Tundi Songani) na Chalinze katika maeneo ya (Kibiki na
Mpera), ambayo Watanzania wote wakiwamo watumishi wa umma, wafanyakazi wa
kampuni binafsi na wajasiriamali wanaweza kupata fursa ya kukopeshwa viwanja
hivyo vilivyopimwa na vyenye hati na kuidhinishwa na mamlaka zote za Serikali
kupitia kwa wabia wao wa kibiashara.
Kwa viwanja vinavyoendelea kukopeshwa, wilayani Kilwa eneo
la Msakasa kilomita moja ya mraba inauzwa kwa Sh 2000, Chalinze ni Sh 4500,
Bagamoyo Sh 10,000, Kigamboni Sh 10,000 na Kibaha mkoani Pwani mita ya mraba
itapatikana kwa Sh 9000.
No comments:
Post a Comment