Na Mwandishi Wetu, Dar es Salaam
MDAU wa muziki wa dansi Tanzania ambaye pia ni Mchumi wa
Chama Cha Mapinduzi CCM, Kata ya Makumbusho, Yusuphed Mhandeni, amesema kuna
haja kubwa wadau kuliunga mkono tamasha la Handeni Kwetu linalotarajiwa
kufanyika Desemba 13, wilayani Handeni, mkoani Tanga ili kuchochea kasi ya
maendeleo na kukuza uchumi wa nchi.
Mdau wa muziki wa dansi Tanzania, Yusuphed Mhandeni, pichani.
Akizungumza mwishoni mwa wiki jijini Dar es Salaam, Mhandeni
alisema kitendo cha kufanyika tamasha hilo na mengineyo makubwa Tanzania,si tu kinachangia
kwa kiasi kikubwa kuitangaza sanaa na utamaduni wa Mtanzania, bali pia kunaleta
maendeleo makubwa.
Alisema tamasha la
Handeni linafanyika katika eneo ambalo wananchi wake na viongozi kwa kiasi
kikubwa wanapambania maendeleo, hivyo ni jambo la busara kuendelea kubuni matukio
makubwa, sanjari na kushirikiana kwa kiasi kikubwa.
Mhandeni alisema nyumba za wageni, hoteli, migahawa na
vyombo vya usafiri vinafanya biadhara kubwa kutoka kwa wananchi wanaohudhuria
tamasha hilo, wakiwamo wasanii na vikundi vingi vinavyonufaika kwa uwapo wa
tamasha hilo.
“Naungana na Watanzania wazalendo wakiwamo waandaaji wa
tamasha kubwa la Handeni Kwetu, linaloandaliwa chini ya mratibu wake mkuu Kambi
Mbwana, huku likipangwa kufanyika Desemba 13 mwaka huu wilayani Handeni mkoani
Tanga kwasababu napenda maendeleo ya nchi yetu.
“Wengine waliunge mkono wakiwamo wafanyabiashara wakubwa,
mashirika na kampuni mbalimbali za Tanzania kwa ajili ya kufaninisha maendeleo
ya Taifa letu, ukizingatia kuwa ili tusonge mbele tunapaswa kuunga mkono juhudi
kama hizi,” alisema Mhandeni.
Mhandeni ni miongoni mwa wadau wanaolipigia chapuo tamasha
la Handeni Kwetu kwa kupitia mabasi yake ya Phed Trans yanayokwenda Mkata,
wilayan Handeni, bila kusahau SmartMind
& Partners iliyopo chini ya Anesa Co. Ltd kwa kupitia kitabu chao cha Ni
Wakati wako wa Kung’aa, Handeni Kwetu Foundation, Wait & Watch Film Company
Ltd, Qs Mhonda J Apex Group of Companies Ltd na Skyblue Security and Risk Mgt
Ltd.
Tamasha la Handeni Kwetu ni
miongoni mwa matukio makubwa ya kiburudani mkoani Tanga, ambako zaidi ya watu
500 walihudhuria tamasha hilo ambalo kwa mwaka huu mipango kabambe ya
kuhakikisha kuwa linafanyika kwa mafanikio.
No comments:
Post a Comment