https://tpc.googlesyndication.com/simgad/8045142562622600543


Recent Post

Sunday, May 28, 2017

Tanzania yatumia Siku ya Afrika Saudi Arabia kutangaza utamaduni wake

Balozi wa Tanzania nchini Saudi Arabia akifurahia chakula cha asili ya Tanzania na mabalozi wa nchini nyingine katika maadhimisho ya Siku ya Afrika nchini hapa yaliyofanyika hivi karibuni.

Na Mwandishi Wetu, Riyadh
Balozi wa Tanzania UBALOZI wa Tanzania nchini Saudi Arabia, uliungana na ofisi nyingine za balozi za nchi mbalimbali kusherehekea Maadhimisho ya Siku ya Afrika yaliyofanyika hivi karibuni nchini Saudi Arabia.


Maadhimisho hayo yalikwenda sambamba na kutangaza utamaduni, ambapo kwa Tanzania, shamra shamra hizo zilikonga nyoyo za wahudhuriaji wengi, ambapo wanafunzi wa Tanzania wanaosoma nchini hapa waliimba nyimbo za kuisifu na kuipamba Tanzania.
Wanafunzi wa kitanzania baada ya kutumbuiza nyimbo za kuisifu Tanzania.
Balozi wa Tanzania nchini Saudi Arabia, aliuambia Mtandao huu kuwa kusudio la kuungana na mabalozi wengine lilifanikiwa kwa sababu lengo halisi ni kuitangaza Afrika na nchi zao, ambapo anaamini kwa maadhimisho hayo nchi yake imepiga hatua kujitangaza kwa kuonyesha utamaduni wao kwa kupitia, ngoma, nyimbo, ngojera, maonesho ya mavazi na maonesho ya vyakula vya asili vya nchi zilizoshiriki,
Wakati wa Maakuli. Balozi wa Tanzania nchini Saudi Arabia akiwa ameshika sahani ya chakula katika maadhimisho ya Siku ya Afrika ambapo vyakula vya asili, ngoma na utamaduni wa Tanzania ulionyeshwa katika tukio hilo.

No comments:

LinkWithin

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...