https://tpc.googlesyndication.com/simgad/8045142562622600543


Recent Post

Thursday, August 03, 2017

Moses Matagili akabidhiwa Milioni 20 zake


Na Mwandishi Wetu, Dar es Salaam

WAENDESHAJI wa bahati nasibu ya Biko ‘Ijue Nguvu ya Buku’, leo wamemkabidhi jumla ya Sh Milioni 20, mshindi wao wa droo ya 28, Moses Matagili, mkazi wa Goba, aliyetangazwa jana Jumatano, jijini Dar es Salaam.
Moses Matagili mshindi wa Biko wa Milioni 20 mkazi wa Goba, katikati akipokea fedha zake kutoka kwa Mratibu wa Matukio na Mawasiliano wa Biko, Hassan Melles kulia, huku akishuhudiwa na afisa wa NMB, tawi na Bank House, jijini Dar es Salaam leo mchana.
 

Matagili anakuwa mshindi wa droo ya 28 ya Biko, inayochezwa kwa njia ya ujumbe mfupi wa maandishi kwa kufanya miamala kwenye simu za M-Pesa, Tigo Pesa na Airtel Money kuanzia Sh 1,000 na kuendelea, huku namba ya kampuni ikiwa ni 505050 na kumbukumbu ni 2456.


Akizungumza mara baada ya kukabidhiwa fedha zake, Matagili anayejishughulisha na kazi za ujenzi wa nyumba, alisema amepokea ushindi wake kwa furaha, baada ya kuuwazia kwa muda mrefu na kuamua kuwa mchezaji mzuri wa Biko.
Mshindi wa droo ya 28 ya Biko, Moses Matagili, kushoto akipokea fedha zake jumla ya Shilingi Milioni 20 kutoka kwa Mratibu wa Matukio na Mawasiliano wa Biko, Hassan Melles kulia katika benki ya NMB leo jijini Dar es Salaam.


Mshindi wa Biko wa Milioni 20, Moses Matagili akiwa anafurahia fedha zake saa chache baada ya kukabidhiwa leo katika benki ya NMB, jijini Dar es Salaam.




Alisema makabidhiano hayo ya fedha yamefanyika haraka, tofauti na matarajio yake, ikiwa ni siku moja baada ya kupigiwa simu ya ushindi na Balozi wa Biko, Kajala Masanja.


“Nashukuru kwa kushinda na kukabidhiwa fedha zangu mapema, nikiamini kuwa nitapiga hatua kubwa kiuchumi kwa namna moja ama nyingine, ukizingatia kuwa ndio matarajio yangu.


“Nawaomba Watanzania wote waendelee kucheza Biko mara nyingi zaidi na wasikate tamaa, kwa sababu kushinda kwangu kumeniongezea imani kubwa kwa waendeshaji wa Biko,” Alisema.


Naye Mratibu wa Matukio na Mawasiliano wa Biko, Hassan Melles, alisema Biko inaendelea kutoa fedha mbalimbali kuanzia Sh 5,000, 10,000, 20,000, 50,000, 100,000, 500,000 na Sh Milioni moja zinazolipwa papo hapo kupitia simu za washiriki waliocheza Biko.


“Biko tunaendelea kulipa fedha mbalimbali za papo kwa hapo pamoja na droo kubwa ya Jumatano na Jmapili ambayo ni Sh Milioni 20, kama tulizompa leo mshindi wetu wa Goba,” Alisema Melles huku akiwataka Watanzania waendelee kucheza Biko ili waibuke na zawadi mbalimbali.


Wakati mshindi huyo akipokea fedha zake, tayari mshindi wa droo ya 27, Viane Kundi, mkazi wa Iringa Mjini naye akiwa ameshapokea fedha zake Jumatatu iliyopita, huku pia mwezi Mei na Juni pekee Biko wakiwa wameshatoa zawadi zaidi ya Sh Bilioni moja.

No comments:

LinkWithin

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...