https://tpc.googlesyndication.com/simgad/8045142562622600543


Recent Post

Sunday, August 06, 2017

Innocent Nyalia wa Dodoma achomoza na Milioni 20 za Biko

Na Mwandishi Wetu, Dar es Salaam
MKAZI wa Dodoma nchini Tanzania, Innocent Nyalia, ameibuka na ushindi mnono wa Sh Milioni 20 kutoka kwa waendeshaji wa Bahati Nasibu ya Biko ‘Ijue Nguvu ya Buku’, katika droo iliyochezeshwa leo jijini Dar es Salaam.
Droo hiyo ilichezeshwa na Balozi wa Biko, Kajala Masanja na Mwakilishi wa Bodi ya Michezo ya Kubahatisha Tanzania, Jehud Ngolo, ambaye kwa pamoja alishuhudia kupatikana kwa mshindi huyo wa droo ya 29 ya Biko.

Akizungumza katika droo hiyo, Mratibu wa Masoko na Mawasiliano wa Biko, Hassan Melles, alimpongeza mshindi huyo wa mjini Dodoma, Nyalia na kuwataka Watanzania wote kuchangamkia fursa za mamilioni ya Biko.

Alisema huu ni wakati wa kutajirika kwa kuvuna mamilioni ya Biko yanayoendelea kutolewa kwa wingi, ikiwa ni mwendelezo wa kuona wachezaji hao wanaotumia simu za M-Pesa, Airtel Money na Tigo Pesa kwa kuingiza namba ya kampuni 505050 na kumbukumbu 2456 wananeemeka na Biko.

“Kama kawaida yetu ushindi wa Biko ni rahisi kupatikana na kucheza kwake kuliko michezo mingine yoyote, hivyo tunawaomba Watanzania wasilaze damu katika mchezo wetu wa Biko unaozidi kutoa mamilioni ya fedha.
“Mbali na ushindi mkubwa wa Sh Milioni 20 unaopatikana Jumapili na Jumatano, pia zipo zawadi za papo kwa hapo kuanzia Sh 5,000, 10,000, 20,000, 50,000, 100,000, 500,000 na Sh Milioni moja zinazolipwa moja kwa moja kwa kupitia simu zao walizotumia kuchezea,” Alisema Melles.

Naye Ngolo, mwakilishi wa Bodi ya Michezo ya Kubahatisha Tanzania, aliendelea kuwakumbusha Watanzania jinsi ya kutumia muda wao kwa kucheza mchezo wa Biko ili wajipatie maendeleo makubwa kutoka Biko.

“Wakati Bodi yetu ikiwapongeza washindi wote wanaoshinda zawadi kubwa na ndogo kutoka Biko, pia nitumie muda huu kuwataka kila mmoja kuona fursa ya michezo ya kubahatisha hususan wa Biko ambao unachezwa kwa kufuata taratibu zote za nchi yetu,” Alisema.

Kwa kutangazwa kwake mshindi, sasa mkazi huyo wa Dodoma anatarajiwa kukukabidhiwa mamilioni yake mapema wiki hii ili aziweke katika matumizi yake ya kawaida katika hali ya kukuza uchumi wake, ikiwa ni siku chache baada ya mshindi wa droo ya 28, Moses Matagili, mkazi wa Goba, kupokea fedha zake wiki iliyopita jijini Dar es Salaam.

No comments:

LinkWithin

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...