https://tpc.googlesyndication.com/simgad/8045142562622600543


Recent Post

Tuesday, August 08, 2017

Innocent Nyeriga: Milioni 20 za Biko nitajengea nyumba

Mshindi wa Droo ya 29 ya Biko, Innocent Nyeriga wa pili kutoka kulia akipokea fedha zake kutoka kwa Mratibu wa Matukio na Mawasiliano wa Biko, Hassan Melles wa pili kutoka kushoto mwenye fulana ya Biko.


Na Mwandishi Wetu, Dodoma
KUTOKANA na changamoto nyingi za ukosefu wa makazi ya kuaminika kwa watu wengi, mshindi wa Sh Milioni 20, Innocent Nyeriga, amesema anatafakari fedha zake alizokabidhiwa jana mjini Dodoma aziweke kwenye ujenzi wa nyumba.

Nyeriga mkazi wa Dodoma na mshindi wa Biko droo ya 29 iliyochezeshwa mwishoni mwa wiki jijini Dar es Salaam, alikabidhiwa fedha zake jana Jumatatu katika benki ya NMB, Mjini Dodoma tayari kwa kuanza kuzitumia kwa matumizi yake ya kawaida.

Akizungumza kwa furaha kubwa, Nyeriga anayejighulisha na kibarua cha kuhudumia mifugo mjini Dodoma, alisema kwamba lengo lake haswa ni kujenga nyumba nzuri ili familia yake iondokane na changamoto ya ukosefu wa makazi bora.
Shughuli ya makabidhiano ya Sh Milioni 20 kwa mshindi wa Dodoma, Innocent Nyeriga ikiendelea katika benki ya NMB jana mjini Dodoma.


Mratibu wa Matukio na Mawasiliano wa Biko, Hassan Melles kushoto akimkabidhi mshindi wao wa Sh Milioni 20 fedha zake jana Jumatatu katika benki ya NMB, Mjini Dodoma anayejulikana kwa jina la Innocent Nyeriga aliyeibuka kidedea kwenye droo ya 29

Mshindi wa Sh Milioni 20 wa mjini Dodoma, Innocent Nyeriga, akiwa amezilalia fedha zake baada ya kukabidhiwa jana Jumatatu katika benki ya NMB, mjini Dodoma. Nyeriga aliibuka mshindi wa Biko droo ya 29.
.
“Nawashukuru Biko bahati nasibu iliyokomboa maisha yangu, hivyo fedha hizi tangu mwanzo nilizipanga nijengee nyumba saa chache baada ya kupewa taarifa ya ushindi wangu, nikiamini haya yote yameletwa na Mungu kwa kuwatumia Biko,” Alisema Nyeriga.


Naye Mratibu wa Matukio na Mawasiliano wa Biko, Hassan Melles, alisema mchezo wa Biko ni mzuri na rahisi kucheza pamoja na kushinda kwake, huku akiwataka Watanzania kuchangamkia ili waweze kuvuna mamilioni ya zawadi kwa kuanzia zile papo kwa hapo bila kusahau donge nono la Jumatano na Jumapili la Sh Milioni 20 kama alizonyakua Nyeriga.


“Mchezo huu wa Biko unachezwa kwa kutumia simu za Tigo Pesa, M-Pesa na Airtel Money ambapo wanachotakiwa ni kufanya miamala kuanzia Sh 1,000 na kuendelea, huku namba ya Kampuni ikiwa ni 505050 na kumbukumbu ni 2456.


“Mbali na kushinda zawadi kubwa ya Sh Milioni 20 ambayo ni lazima iende kwa mshindi Jumatano na Jumapili, lakini pia zawadi za papo kwa hapo zinatoka kila dakika ambazo ni zile za Sh 5,000, 10,000, 20,000, 50,000, 100,000, 500,000 na Sh Milioni moja inayoenda kwa mshindi mara baada ya kupokea ujumbe wa ushindi kwenye simu anayotumia kuchezea Biko,” Alisema Melles.


Kwa kukabidhiwa fedha zake mshindi wa Dodoma, mshindi mwingine wa Milioni 20 anatarajiwa kujulikana katika droo ya kesho Jumatano maarufu kama Jumatamu na nyingine itakuwa Jumapili huku ikiitwa Jumadili na waendeshaji hao wa Biko.

No comments:

LinkWithin

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...