Na Mwandishi Wetu, Dar es Salaam
MSHINDI wa Sh Milioni 10 wa droo ya nne ya mchezo wa kubahatisha wa Biko IJue Nguvu ya BUku, Emmanuel Philipo, ametangaza rasmi nia yake ya kuuaga umsikini baada ya kukabidhiwa fedha zake jumla ya Sh Milioni 10.
Makabidhiano hayo yalifanyika jana jijini Dar es Salaam kwa kuhudhuriwa na baadhi ya wataalam wa benki ya NMB kwa ajili ya kumuelimisha mashindi huyo wa bahati nasibu ya Biko ili azitumie vizuri fedha zake.
Akizungumza jana jijini Dar es Salaam, Philipo alisema kwamba ni wakatiwake
wa kuuaga umasikini kwa sababu amepata nafasi ya kutimiza ndoto zake kiuchumi kwa kuhakikisha kwamba anakamilisha mradi wake wa garage ya kutengenezea magari katika viunga vya jiji la Dar es Salaam.
Meneja Huduma kwa Wateja wa Biko, Grace Kaijage akionyesha namba za
kucheza bahati nasibu yao inayofanikisha ushindi wa mamilioni kutoka kwa
Watanzania, ambapo droo iliyopita alitangazwa Emmanuel Philipo ambaye
jana alipewa kiasi cha Sh Milioni 10.
Alisema fedha alizopata jumla ya Sh Milioni 10 ni nyingi,
huku akizipata kwa sababu ya kushiriki bahati nasibu ya Biko, akiamini
kuwa ni mpango wa Mungu kumpatia fedha hizo ukizingatia kuwa ni wengi
wanaocheza bahati nasibu.
"Namshukuru
Mungu kwa kuniletea zawadi hii kwa kuwatumia wachezeshaji wa biko,
hivyo ni wakati wangu wa kufanikiwa kimaisha kwa sababu ndio dhamira
yangu kuu kupiga hatua kubwa kimaendeleo kwa kuamua kucheza bahati
nasibu hii kwa njia yaujumbe wa maandishi kwa kufanya muamala kwenye
simu za Tigo, Vodacom na Airtel ambapo namba ya kampuni niliweka 505050
na ile ya kumbukumbu niliingiza 2456 na kutangazwa mshindi mwishoni mwa
wiki.



















