https://tpc.googlesyndication.com/simgad/8045142562622600543


Recent Post

Wednesday, September 14, 2016

Waimbaji 10 wa injili waingia fainali


Kikundi cha Makerubi kutoka Manyara ambao walijiandikisha wakitokea Temeke waliweza kufanikiwa kuingia hatua ya nusu fainali katika shindano la Gospel Star Search 2016 kwa kuweza kuimba kwa ustadi mkubwa. Shindano la Nusu fainali lilifanyika katika viwanja vya Biafra - Kindononi jijini Dar es Salaam mwishoni mwa wiki iliyopita.

Na Cathbert Kajuna wa Kajunason blog.

Vijana 10 wamefanikiwa kuingia hatua ya fainali katika shindano la kumtafuta mkali wa kuimba nyimbo za injili 'Gospel Star Search 2016' lililofanyika katika viwanja vya Biafra jijini Dar es Salaam.

Akizungumza Meneja Mradi wa Gospel Star Search 2016, Samwel Sasali alisema kuwa ni vyema vijana wakazingatia mafundisho yote waliyopatiwa na walimu wao ili waweze kushindana kwa uweledi na ustadi wa hali ya juu. Alisema wakati umefika wa vijana kutambua talanta au vipaji walivyopewa na mwenyezi Mungu ili viwaletee manufaa katika kumtangaza Bwana Yesu Kristo.

"Tokea tumeanza kuzunguka kukusanya vijana hakika tumeweza kupata vijana wengi wenye vipaji na kuonyesha kuwa mwamko wa vijana katika kutambua vipaji vyao umekuwa mkubwa, hakikuwa jambo jepesi sana ila yote kwa yote tunamshukuru Mwenyezi Mungu aliyeweza kufanikisha yote",  alisema Sasali.


Umati wa watu waliohudhuria shindano la Gospel Star Search lililofanyika mwishoni mwa wiki iliyopita katika viwanja vya Biafra - Kinondoni jijini Dar es Salaam.
Mshiriki namba 4. Grace Madole akiimba katika jukwaa la Gospel Star Search lililofanyika mwishoni mwa wiki iliyopita katika viwanja vya Biafra - Kinondoni jijini Dar es Salaam. Mshiriki huyu hakuweza kupenya hatua ya fainali.
Mshiriki namba 5. Winnypraise William akiimba katika jukwaa la Gospel Star Search lililofanyika mwishoni mwa wiki iliyopita katika viwanja vya Biafra - Kinondoni jijini Dar es Salaam. Mshiriki huyu alipenya kuingia hatua ya fainali.
Shindano la Gospel Star Search lilikuwa ni vuta nikuvute pamoja na mshiriki namba 6. Willansia Lema kuimba kwa hisia ila hakuweza kufanikiwa kuingia hatua ya nusu fainali ambayo iliweza kuingiza washiriki wapatao 10 na kufanya washirikiki watano (5) kuaga mashindano.
Mshiriki namba 10. Flora Kachema alifanikiwa kuingia fainali.
Majaji wa shindano la Gospel Star Search (GSS) kutoka kulia ni Mchungaji Sam Mwangati, Sarah Ndossi na Fred Msungu wakiwa wamenyanyuka kuonyesha heshima ya pekee kwa mshiriki ambaye aliweza kuvuta hisia zao.
Mshiriki Mdogo kuliko wote akiwa aliwavuta hisia majaji wakajikuta wanatoa heshima ya pekee kwa kusimama.
Wageni waliohudhuria shindano hilo wakifurahia kwa shangwe.
Nderemo na vifijo vilitawala.
Mshiriki huyo akiwa amewateka na kujikuta wakiimba kwa hisia wageni waliohudhuria.
Mshiriki Sunday Lunkombe alifanya vyema kuliko wenzake na kufanikiwa kuongoza hakua ya kuingia fainali kwa kujizolea alama nyingi.
Washiriki wakionyesha umahili wa kuimba pamoja kabla ya kutangazwa kumi bora.

Meneja Mradi wa Gospel Star Search 2016, Samwel Sasali akionyesha vijana walifanikiwa kuingia hatua ya fainali (kumi Bora) mara baada ya mchuano mkali.
Kiongozi wa Majaji, Mchungaji Sam Mwangati akisoma majina ya vijana walifanikiwa kuingia hatua ya fainali ya shindano la Gospel Star Search 2016 lililofanyika katika uwanja wa Biafra - Kinondoni jijini Dar es Salaam mwishoni mwa wiki iliyopita. Fainali za shindano hili zinatarajiwa kufanyika jumapili ya Septemba 18, 2016 katika ukumbu wa Milado, Sinza jijini Dar es Salam.

Aliongeza kuwa shindano la Gospel Star Search 2016 liliweza kupata  washiriki wengi ila wakafanyiwa mchujo na kupatikana wapatao 15 ambao  waliweza kuingia hatua ya nusu fainali na wakafanya mchuzo katika  viwanja vya Biafra wakapatikana 10 ambao wameingia katika kikaango na  ipatapo Septemba 18, 2016 Jumapili katika ukumbi wa Milado, Sinza ndipo  fainali zitakapofanyika.

Vijana 15 waliokuwa wameingia nusu fainali ni 1. Makerubi,  2. Enighenja Mmbaga, 3. Upendo John, 4. Grace Madole,   5. Winnypraise William, 6. Willansia Lema, 7. Rogate Kalengo, 8. Suleiman Wilson, 9. Innocent Eliya. Wengine ni 10. Flora Kachema, 11. Steve Njama, 12. Winnifrida Dudu, 13. Calvin John, 14. Sunday Lunkombe na 15. Beda Andrew.

Waliofanikiwa kuingia Fainali ni vijana 10 ambao ni 1. Makerubi, 2. Beda Andrew, 3. Winnypraise William, 4. Rogate Kalengo, 5. Suleiman Wilson, 6. Flora Kachema. Wengine ni 7. Steve Njama, 8. Winnifrida Dudu, 9. Calvin John na 10. Sunday Lunkombe.

Shindano la GSS limedhaminiwa na Maendeleo Bank,  Grace Product, Brand exponetial, Kiango media, Clouds Media Group, Fm studios (Faith music lab) na 3D. 

No comments:

LinkWithin

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...