Na Mwandishi Wetu, Dar es Salaam
“IKIWA hujawahi kupata tatizo huwezi jua kama wapo binadamu
wenzetu wanaotabika kusaka dawa au vitu vinavyoweza kuwaondoshea maswahibu yao
yanayoendelea kuwapa wakati mgumu katika maisha yao bila kuangalia wanaishi kwa
mtindo gani,”. Ndivyo alivyoanza kusema Sheikhe Hussein Msopa maarufu kama
Sharifu Majini.
Chifu Hussein Msoma maarufu kama Sheikhe Sharifu Majini akiwa katika majukumu yake ya kawaida kama anavyoonekana pichani.
Ndio, sheikhe huyo mwenye maskani yake Mabibo Mwisho, jijini Dar es Salaam, unaweza kushangazwa na idadi kubwa ya watu wanaotembelea katika ofisi ya sheikhe hiyo, huku kila mmoja wake akiwa na shida yake inayohitaji utatuzi. Kwa wale ambao hawajui lolote kuhusu sheikhe Sharifu majini, pindi wanapopita katika mtaa huo, wanaweza kudhani labda kuna harusi, msiba ayu shughuli yoyote ya kijamii kutokana na ingia tokay a watu katika nyumba ya sheikhe huyo inayotoa huduma mbalimbali za kuombea watu, kuwapatia dawa zikiwamo zinazohusiana na mambo ya majini.
Ndio, sheikhe huyo mwenye maskani yake Mabibo Mwisho, jijini Dar es Salaam, unaweza kushangazwa na idadi kubwa ya watu wanaotembelea katika ofisi ya sheikhe hiyo, huku kila mmoja wake akiwa na shida yake inayohitaji utatuzi. Kwa wale ambao hawajui lolote kuhusu sheikhe Sharifu majini, pindi wanapopita katika mtaa huo, wanaweza kudhani labda kuna harusi, msiba ayu shughuli yoyote ya kijamii kutokana na ingia tokay a watu katika nyumba ya sheikhe huyo inayotoa huduma mbalimbali za kuombea watu, kuwapatia dawa zikiwamo zinazohusiana na mambo ya majini.
Sheikhe Sharifu Majini pichani.
Watu wanaweza kushangaa au kujiuliza. Je, ni kweli mtu mwenye
tatizo anaweza kupata ufumbuzi wa shida yake atakapomuona sheikhe huyo? Katika
mazungumzo na mtandao huu yaliyofanyika wiki iliyopita, sheikhe Sharifu anasema
kwamba amedhamiria kuwakomboa wale wenye mahitaji na matatizo yanayohusu
majini, ukosefu wa uzazi kwa njia za ushirikiana, kusumbuliwa na majini pamoja
na kuzitafsiri ndoto mbalimbali zinazohusiana na mifumo ya maisha ya mwanadamu. Sheikhe huyo anasema kwamba uamuzi wake wa kuamua
kujihusisha na masuala hayo umetokana na kufahamu adha kubwa inayowakumba
binadamu, jambo linalowafanya waishi kwa mashaka katika kipindi chote cha
maisha yao.
“Mtu anaweza kwenda hospitali kufanya uchunguzi wa afya ya
matatizo ya uzazi na kukuta hana tatizo lolote. Lakini kila anavyojitahidi ili
ashike mimba kwa ajili ya kufurahisha nafsi au ndoa yake anajikuta anashindwa
kufanikiwa.
Hapo ndipo mtu anapotakiwa kuangalia njia nyingine ikiwamo
dua kulingana na imani yake, maana tiba ya kwanza ya mtu ni imani yake, hivyo
anapoamua kuja kwa Sharifu majini nafanya wajibu wangu kuangalia mhusika
anatatizwa na jambo gani, yakiwamo majini ambayo mara kadhaa hufikia kuwazuia
watu kushika mimba,” alisema Msopa.
Anasema mbali ya kushika mimba, baadhi ya wanawake wakati
mwingine hujifungua na watoto wao kufariki au hata mimba zao kuharibika mara
kwa mara zinazochagizwa na majini wabaya ambao huwasumbua wanawake wengi. Kwa mujibu wa Sheikhe huyo, baadhi ya majini pia huwafunga
au kuwadhibiti wanawake wasipate watoto aidha wa kiumbe au wa kike, hivyo jambo
kama hilo nahakikisha kwamba nayatoa majini hayo na kuwafungua akina mama hao
ambao wengi wao hujikuta wakipoteza matumaini.
Mbali na mambo ya uzazi, shekhe Sharifu majini anasema
kwamba wapo watu wanaoishi kwa wasiwasi na hawaoni faida katika maisha yao
hususan katika shughuli zao za kijamii kutokana na kusumbuliwa na changamoto
mbalimbali. “Haya mambo yapo na yanatuhusu sisi wanadamu, hivyo ni budi
jamii kuelewa kwamba katika kitu kianchoitwa jinni si kigeni kwasababu tunaishi
nacho ingawaje hatujapewa uwezo wa kukiona kiumbe hicho kwa macho yetu. “Hawa viumbe hutusumbua sana na hugawawanyika katika makundi
mawili, yani wale wabaya na wazuri ambao mtu anapotaka kufahamu haya kwa kina
au juu ya tatizo lake linalomsumbua namkaribisha ofisini kwangu Mabibo,
nikiamini kuwa hatua hii inaweza kuwafanya watu waishi kwa amani na kufanikisha
yale waliyokusudia,” alisema.
Sheikhe Majini anasema katika kutoa elimu ya majini na
kuombea watu wenye shida, amedhamiria kutoa elimu hiyo haswa kwa wanawake
Oktoba 30, katika Ukumbi wa Diamond Jubilee, kuanzia saa 1 asubuhi hadi saa 12
za jioni.
Sheikhe huyo anasema kwamba katika dua hiyo kwa akina mama
na kuwapa ushauri kwa wale watakaokuwa na matatizo hakutakuwa na kiingilio
chochote kwenye ukumbi huo mkubwa na marufu hapa jijini Dar es Salaam. Msopa anasema ameamua kuandaa kongamano hilo la dua kwa
akina mama baada ya kuona wenye uhitaji huo ni wengi na hawatoshi kufanyia
katika eneo la ofisi yake baada ya kujaribu kufanya hivyo hivi karibuni na
kujaza watu wengi. Mbali na kushindwa kutoa huduma hiyo kwa wakati, pia
aligundua si sahihi kuwajaza watu wengi katika eneo dogo hali inayoweza kuibua
matatizo mengine, ndio maana akaona safari hiii, yani Oktoba 30 apeleke
kongamano hilo katika ukumbi wa Diamond Jubilee.
Anasema kwamba mambo hayo anayafahamu vizuri baada ya
kujikita kwa muda mrefu, huku akiwa na kipaji cha aina yake cha kutambua namna
ya kutatua tatizo la binadamu lililosababishwa kwa njia za ushirikina au majini
ambayo ndio kesi nyingi zinazowatatiza
binadamu.
“Naomba akina mama wengi waje Diamond Jubilee Oktoba 30
katika kongamano langu ambalo naliandaa kwa mapenzi makubwa kwa watu wote
nikiamini kuwa safari hii tutakuwa na wigo mpana wa kutoa huduma zangu kutokana
na uzoefu wangu na kipaji nilichokuwa nacho.
“Watu wengi huhangaika sehemu mbalimbali kutafuta suluhu ya
matatizo yao, lakini wakija kwangu Mabibo Mwisho ambapo kila mtu ukimuuliza kwa
sheikhe Sharifu majini anakuelekeza au kukuleta wanajikuta wanapata tiba
halisi,” alisema Msopa au Sharifu Majini kama anavyojulikana na wengi, huku
ofisi yake ikipatikana Mabibo mwisho.
Sheikhe Sharifu Majini mwenye asili ya wilayani Handeni,
mkoani Tanga, pia ajihusisha na elimu za nyota, tafsiri za ndoto, bahati,
kuondoa mikosi pamoja na matatizo mbalimbali yanayowasumbua binadamu, hususan
yale yanayoingia kwa njia za kienyeji.
No comments:
Post a Comment