Na Mwandishi Wetu, Tanga
WAZIRI wa maji Mhandisi Gerson Lwenge, pichani juu ameombwa kuingilia kati na kushughulikia kwa haraka utata uliogubika utekelezaji wa mradi wa Bwawa la maji la malezi lilipo kata ya Malezi ,Mjini Handeni ambao haujaanza licha ya Benk ya Dunia kutoa shs. Milioni 700 kwa ajili ya mradi huo.
WAZIRI wa maji Mhandisi Gerson Lwenge, pichani juu ameombwa kuingilia kati na kushughulikia kwa haraka utata uliogubika utekelezaji wa mradi wa Bwawa la maji la malezi lilipo kata ya Malezi ,Mjini Handeni ambao haujaanza licha ya Benk ya Dunia kutoa shs. Milioni 700 kwa ajili ya mradi huo.
Wakizungumza katika mahojiano na
wawakilishi wa vyombo vya habari waliokuwa wanafuatilia utekelezaji wa
mradi huo,
wakazi hao ambao wanalazimika kutembea kilometa zaidi ya 5 kufuatilia
maji katika vyanzo vya maji wamesema hawaoni
sababu ya mradi huo kutokuanza licha ya fedha hizo
kutolewa.
Kitombo alisema kwa taarifa
alizonazo mwaka 2013 Benki ya Dunia iliingiza sh. Milioni 400 kwa ajili ya
ujenzi wa bwawa hilo ambao unatarajiwa
uwanufaishe Wakazi Zaidi ya 6000.
Gharama za ujenzi wa bwawa hilo ni sh. Milioni 880.
Aliendelea kueleza kuwa mwaka jana
sh. Milioni 300 zilliingizwa katika akaunti na kufanya jumla ya fedha
zilizoingizwa katika akaunti ni shs. Milioni 700
Pia alieleza mshangao wake kwa
nini
mradi huo bado unaendelea kutekelezwa na Halmshauri ya Wilaya wakati ambapo
eneo la mradi liko Halmashauri ya Mji.
(Pichani ni Mbunge wa
Jimbo la Handeni Mjini,Omari Kigoda)
Naye Afisa Mtendaji wa Kata hiyoya
Malezi. Muhaji Ramadhani Mlaki alisema kuwa mara nyingi amepokea wataalamu
ambao wanakuja kuona eneo lakini hakuna kinachoendelea baada ya hapo licha ya
kuwaambia watu wenye maeneo yao ambayo yameingizwa kwenye mradi huo waache
kulima.
“Tunapata lawama kwa wananchi kwa
sababu tunawalewesha hadi mwisho wanatuambia kuwa na sisi tumekuwa wanasiasa,”
alisema.
Naye Cecilia Ibrahimu wa
Malezi Kwedinguzo ambaye ana shamba kwenye eneo hilo la mradi wa bwawa
alikubali kutoa eneo lake kwa sababu maji ni kero inayowagusa watu
wote. “Sina cha kusema nataka maji tu.
Cha
ajabu tuliambiwa tutapewa mashamba na kusaidiwa kulimiwa lakini mpaka sasa
hatujaonyeshwa mashamba na mradi haujaanza,’ alisema Bi.
Cecilia.
Mwenyekiti wa Jumuiya ya Wazazi
katika Kata hiyo, Mzee Abdallah Kombo walipoingia katika uongozi kilio ni hicho
hicho hadi hivi sasa. Alisema kuwa wananchi wanategemea malambo madogo
yaliyochimbwa kwa juhudi za Mbunge wa zamani wa Handeni, marehemu Abdallah
Kigoda.
No comments:
Post a Comment