Na Mwandishi Wetu, Kagera
TAASISI ya kifedha ya Bayport Financial Services inayojihusisha na mambo ya mikopo, jana imewakabidhi hundi ya Sh Milioni tatu watoto watatu wilayani Biharamulo, mkoani Kagera, kwa ajili ya kunufaika na huduma ya Bima ya Elimu iliyoachwa na mzee wao Karume Ochieng aliyefariki Dunia, huku akiwa amejiunga na huduma ya bima kwa ajili ya watoto wake hao.Mratibu Mauzo wa Bima ya Elimu wa Taasisi ya Kifedha inayotoa Mikopo(Bayport Financial Services, Ruth Bura akikabidhi mfano wa hundi kwa familia ya marehemu Karume ambaye alikuwa amejiunga na bima hiyo katika shule ya msingi Nyamuhuna iliyopo wilayani Biharamulo mkoani Kagera, kushoto ni Meneja Mauzo wa Bayport Kanda ya Ziwa, Lugano Kasambala. Taasisi hiyo imeanzisha bima ya elimu ili kusaidia kiasi cha ada kwa watu wa karibu walioainishwa na mteja wao endapo atakumbwa na umauti.
Watoto hao ambao wamepewa hundi hiyo itakayowawezesha kila mwaka katika vipindi vya miaka mitatu mfululizo kupewa Sh Milioni moja kwa ajili ya kuwalipia ada katika shule wanazosoma ni pamoja na Athieno Karume, Chacha Karume na Aaptalius Karume.
Makabidhiano ya hundi kwa familia ya marehemu Karume yakiendelea wilayani Biharamulo, mkoani Kagera.
Akizungumza katika makabidhiano ya hundi hiyo kwa watoto hao, Mratibu wa Bima ya Elimu ya Bayport Financial Services, Ruth Bura, alisema kwamba kukabidhi hundi hiyo kutawafanya watoto hao wasome kwa raha, baada ya kuwekewa bima hiyo na marehemu baba yao kutokana na mapenzi mema na vijana hao wanaoendelea na masomo.
Meneja Mauzo Kanda ya Ziwa kutoka Bayaport Financial Services, Lugano Kasambala, akitayarisha mfano wa hundi ya Sh Milioni Tatu kwa ajili ya kukabidhi familia ya marehemu Karume. Mwenye miwani ni Mratibu wa Bima ya Elimu wa Bayport, Ruth Bura.
Alisema Bayport imekuwa ikilipa watu waliotajwa katika huduma ya bima kwenye taasisi yao, wakiamini kuwa huduma hiyo itakuwa na manufaa makubwa na Watanzania wote wenye ndoto za kuona watoto wao wanasoma kwa bidii.
Gari linalomilikiwa na Bayport Financial Services, likiingia katika shule ya Msingi Nyamuhuna, iliyopo wilayani Biharamulo, mkoani Kagera kwa ajili ya kukabidhi hundi ya Sh Milioni Tatu.
"Bayport ni taasisi ya Watanzania wote, hivyo tunaamini kukabidhi hundi hii kwa wanafunzi hawa ni jambo jema litakalowapatia mwangaza zaidi, ukizingatia kwamba kila mwaka tutawapa sh Milioni Milioni moja kwa kipindi cha miaka mitastu mfululizo
.
"Tunaomba watoto hawa watumie fursa hii vizuri na iwe njia moja wapo ya kuwafanya Watanzania wote waendelee kuiunga mkono taasisi hii yenye kutoa huduma bora za mikopo ya fedha, viwanja na, bima ya magari na huduma nyingine muhimu zinazokuza uchumi na kuwakwamua Watanzania wote,” alisema Ruth. Naye Chacha Karume, aliishukuru Bayport kwakuwapatia fedha hizo huku akisitiza kwamba zimekuja wakati muafaka kwa ajili ya kuwakwamua katika kipindi hiki cha kuelekea mwisho wa mwaka.
“Tunashukuru kuona tumepewa fedha hizi bila usumbufu wowote na tunaamini tutasoma vizuri, maana changamoto za ada na huduma nyingine za kijamii zitakuwa zimekombolewa katika kipindi cha miaka mitatu mfululizo tutakapopewa fedha hizo,” Alisema.
Bayport ni taasisi ya kifedha inayotoa huduma bora za kifedha, ambapo imekuwa ikizindua huduma mbalimbali kama vile mikopo ya bidhaa, viwanja vya mradi wa Vikuruti, wilayani Kibaha, mkoani Pwani, mikopo ya fedha na nyinginezo zinazowakwamua kiuchumia wateja wao ambao ni watumishi wa umma na wafanyakazi wa kampuni zilizoidhinishwa na Bayport, huku huduma hizo zikitolewa pia kwa njia ya mtandao wa www.kopabayport.co.tz.
No comments:
Post a Comment