Mkurugenzi wa Sensa na Takwimu za Jamii Ofisi ya Taifa ya Takwimu (NBS), Iphrahim Kwesigabo (kushoto), akizungumza katika mkutano na waandishi wa habari Dar es Salaam leo mchana kuhusu mfumuko wa bei wa Taifa kwa mwezi Agosti, 2015. Kulia ni Kaimu Meneja wa Idara ya Takwimu za Ajira na Bei, Ruth Minja.
Wanahabari wakichukua taarifa hiyo.
Na Dotto Mwaibale
UWEZO wa shilingi 100 ya Tanzania katika kununua bidhaa na huduma umefikia shilingi 62 na senti 97 mwezi Agosti, 2015 kutoka mwezi Septemba, 2010 ikilinganishwa na shilingi 62 na senti 98 iliyokuwa mwezi Julai, 2015.
Hayo yamebainishwa na Mkurugenzi wa Sensa na Takwimu za Jamii Ofisi ya Taifa ya Takwimu (NBS), Iphrahim Kwesigabo wakati akitoa taarifa kuhusu mfumuko wa bei wa taifa wa mwezi Agosti, 2015 kwa waandishi wa habari ofisini kwake Dar es Salaam leo.
Kwesigabo alisema mfumuko wa bei wa mwezi Agosti 2015 unaopimwa kwa kipimo cha mwezi umeongezeka kwa asilimia 0.02 ikilinganishwa na asilimia 0.41 iliyokuwa mwezi Julai, 2015.
"Fahirisi za bei zimeongezeka hadi 158.81 mwezi Agosti, 2015 kutoka 158.78 mwezi Julai, 2015.
Alisema kuongezeka kwa fahirisi za bei kumechangiwa hasa na kuongezeka kwa bei za baadhi ya bidhaa zisizo za vyakula, baadhi ya bei za bidhaa zisizo za vyakula zilizochangia kuongezeka kwa fahirisi ni pamoja na gesi kwa asilimia 2.0, mafuta ya taa kwa asilimia 2.3, mazulia kwa asilimia 1.4, dizeli kwa asilimia 3.8 na petroli kwa asilimia 8.3.
Gwesigabo alisema kuwa mfumuko wa bei wa Taifa kwa kipimo cha mwaka unapima kiwango cha badiliko la kasi ya bei za bidhaa na huduma zote zinatumiwa na kaya binafsi.
Alisema mfumuko wa bei wa taifa kwa mwezi Agosti, 2015 umebaki kuwa asilimia 6.4 kama ilivyokuwa mwezi Julai 2015.
Aliongeza kuwa hali hiyo inamaanisha kuwa kasi ya upandaji wa bei za bidhaa na huduma kwa mwaka ulioishia mwezi Julai, 2015.
Alisema Fahirisi za bei zimeongezeka hadi 158.81 kwa mwezi Agosti, 2015 kutoka 149.31 mwezi Agosti, 2014.
Alisema Mfumuko wa bei wa bidhaa za vyakula na vinywaji baridi kwa mwezi Agosti 2015 umepungua hadi asilimia 10.2 kutoka asilimia 10.6 ilivyokuwa mwezi Julai 2015.
Alisema mfumuko wa bei kwa baadhi ya nchi za Afrika Mashariki mfumuko wa bei nchini una mwelekeo unaokaribiana na baadhi ya nchi nyingine za Afrioka Mashariki ambapo mfumuko wa bei kwa mwezi Agosti 2015 nchini Kenya umefikia asilimia 5.84 kutoka asilimia 6.62 mwezi Julai, 2015 na Uganda umefikia asilimia 4.80 kutoka asilimia 5.4 mwezi Julai, 2015.
No comments:
Post a Comment