Na
Kambi Mbwana, Dar es Salaam
MBUNGE
wa Kigoma Kaskazini, kwa tiketi ya Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema),
Zitto Kabwe, amesema ameanza kuifuatilia sanaa baada ya kuona mateso ya ugonjwa
wa marehemu Juma Kilowoko, maarufu kama Sajuki, aliyezikwa jana, katika
makaburi ya Kisutu, jijini Dar es Salaam na kuhudhuriwa na watu wengi, akiwamo
Rais Jakaya Mrisho Kikwete.
Zitto Kabwe, akizungumza jambo katika makaburi ya Kisutu jana.
Zitto aliyasema hayo jana katika mazishi ya Sajuki, akisema kuwa awali hakuingia zaidi katika undani wa masuala yanayohusu sanaa, ingawa sasa anakili kuifahamu vyema kiasi cha kutamani kuingia kwenye mapambano yanayohusu mambo ya sanaa.

“Sikuwa
naifuatilia zaidi sanaa, lakini baada ya kuona mateso ya Sajuki, hakika
nikaingia kiasi cha kushiriki kucheza filamu ya kuchangisha fedha za kumsaidia
marehemu ambaye kwa mapenzi yake amekwenda mbele za haki.
“Nitashiriki
kuangalia namna ya kuwasaidia wasanii kwa ajili ya kuweka mambo sawa katika
tasnia ya sanaa, maana ina nguvu kama inavyoonekana hapa tunaposhiriki mazishi
ya Sajuki,” alisema Sajuki.
Zitto
ni miongoni mwa wabunge makini wanaoisumbua sana serikali ya Jakaya Mrisho
Kikwete kutokana na kutoa hoja nzito kiasi cha kuwasumbua viongozi na watendaji
wengi serikalini.
No comments:
Post a Comment