Na Kambi Mbwana, Dar
es Salaam
WATANZANIA wamefikia
idadi ya 44,929,002 mwaka 2012 kutoka watu 34,443,603 katika sensa ya watu na
makazi iliyotangazwa jana na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Jakaya
Mrisho Kikwete.
Idadi hiyo ni kubwa na
kumuogopesha Rais Kikwete na kutangaza watu watumie uzazi wa mpango, ikiwa ni
kutokana na kugundulika kuwa jumla ya idadi ya watu wote nchini sasa, ni
milioni 44,929,002, ikiwa ni ongezeko la watu milioni 10 tangu ilipofanyika
Sensa ya mwaka 2002.
Kwa mujibu wa matokeo
hayo, upande wa Tanzania Bara kuna Watanzania milioni 43,625,434, wakati Zanzibar
kuna watu milioni 1,303,568.
Akizungumza baada ya
kufanya uzinduzi huo, Rais Kikwete jana aliwataka Watanzania wahakikishe kwamba
wote wanafuata uzazi wa mpango, akisema kuwa ongezeko hilo ni kubwa na serikali
itashindwa kuwahudumia kama inavyotakiwa.
“Sensa ya mwaka 2002 ilionyesha
kuwa Watanzania tupo milioni 34, lakini hii ya mwaka huu tumefikia milioni 44
na kuonyesha kuwa ni ongezeko kubwa sana.
“Kwa mujibu wa Ofisi
ya Taifa ya Takwimu, Watanzania tutafikia watu milioni 51, ikiwa ni kwasababu
ya watu kuzaliana na ndio maana kuna haja ya kupanga uzazi,” alisema Kikwete.
Wakati Taifa linapata
Uhuru, inakadiriwa kuwa mwaka 1967, Watanzania Bara walikuwa milioni 12.3 wakati
Tanzania Visiwani walikuwa 300,000 ambapo sasa wapo milioni 1,303,568.
No comments:
Post a Comment