Mkuu wa Wilaya Kilindi, Selemani Liwowa
Na Kambi Mbwana, Dar es Salaam
MKUU wa
Wilaya ya Kilindi, mkoani Tanga, Selemani Liwowa, amenusuru kutokea kwa
machafuko ya wakulima na wafugaji katika wilaya yake, baada ya wakulima wa
kijiji cha Mswaki kuwateka ng’ombe waliokuwa kwenye mashamba yao na kuwapeleka
kijijini kama ishara ya kuonyesha uharibifu unaofanywa na wafugaji katika
vijiji vyao.
Hatua
hiyo ilisababisha kutoelewana na kumfanya Mkuu wa wilaya kwenda katika kijiji
hicho wiki iliyopita kwa ajili ya kuangalia tatizo na kuepusha mgogoro huo
unaosumbua katika vijiji vya wilaya Kilindi na Tanzania kwa ujumla.
Akizungumza
na Handeni Kwetu, kwa njia ya simu, DC Liwowa alisema kwa uchunguzi wao umegundua kuwa
baadhi ya wenyeviti wa vijiji vyao wanaruhusu kuingia kwa wafugaji bila kufuata
utaraatibu jambo lililoleta balaa katika kijiji cha Mswaki na Turiani, wilayani
kwake.
Alisema
wakulima hao waliamua kuwachukua ng’ombe hao naa kuwapeleka kijijini kwa ajili
ya kushitaki kwa serikali ya kijiji, lakini baadaye wafugaji hao walibadilisha
na kusema kuwa mifugo yao imetekwa kwa ajili ya kuiba.
“Hili ni
tatizo lililotokea wiki iliyopita na wala sio jipya kama inavyodaiwa, hasa
baada ya wafugaji wanaoachia ng’ombe zao kulalama kwa kusema kuwa mifugo yao
imetekwa na wakulima, hivyo kuleta kutoelewana miongoni mwao.
“Mimi na
ujumbe wangu tulipata fursa ya kwenda katika maeneo yale kuweka mambo sawa,
hivyo tuligundua kuwa baadhi ya wenyeviti wanaruhusu wafugaji kuendelea kuingia
katika sehemu zao bila kuangalia athari zinazoweza kujitokeza,” alisema.
Migogoro
ya ardhi kati ya wakulima na wafugaji imeendelea kuwa tatizo katika wilaya
mbalimbali hapa nchini, jambo linalotakiwa liangaliwe upya na Watanzania wote,
wakiwamo viongozi wa vijiji, Kata, Tarafa na wilaya kwa ujumla.
No comments:
Post a Comment