Na Mwandishi Wetu, Handeni
NYUMBA zaidi ya 37 zimekumbukwa na mafuriko kutokana na mvua kubwa
kunyesha mwishoni mwa wiki katika tarafa ya Sindeni, wilayani Handeni
mkoani Tanga.
Mbali na nyumba hizo, pia bwawa muhimu linalotumiwa na wakazi wa
Sindeni la Msonera, nalo limesombwa na kuwaacha njia panda wananchi
wa Sindeni.
Kwa mujibu wa mashuhuda wa tukio hilo, mvua hiyo imenyesha kwa
zaidi ya saa tatu na kuleta kadhia hiyo, jambo linalowafanya wananchi
hao wahitaji msaada mkubwa kutoka serikalini.
Mwandishi wetu aliyekuwa wilayani Handeni, alitupasha kuwa baada
ya mvua hiyo kunyesha, bwawa lilisombwa pamoja na nyuma 37, huku
ikidariwa kuwa zaidi ya mifugo elfu 70,000 itaathiriwa kwa kuharibiwa
kwa bwawa hilo.
Mkuu wa wilaya ya Handeni, Muhingo Rweyemamu (pchani) , alithibitisha
kutokea kwa mvua hiyo iliyosomba bwawa hilo na kusema wanahitaji
msaada kutoka serikali kuu kwasababu tatizo hilo sio la watu wa
Handeni peke yao.
“NI habari mbaya kwetu wote, maana mvua hii iliyonysha kwa saa
kadhaaa imeleta balaa na kuziacha kaya katika mashaka makubwa,
sambamba na mifugo ambayo huenda ikawa kwenye wakati mgumu kama
hakutakuwa na njia nzuri ya kusaidia.
“Sisi kwa pamoja tutajaribu kushirikiana kwa karibu na wenzetu
wa serikali, ikiwamo ofisi ya Waziri Mkuu ili tupate msaada zaidi,”
alisema Rweyemamu.
Licha ya mvua kuwa jambo la muhimu kwa watu wote duniani, lakini
wakati mwingine huwa inaleta madhara na kuziacha kaya katika wasiwasi
mkubwa hasa pale inapoharibu miundo mbinu mbalimbali na hata mafuriko
yanayoziacha kaya njia panda.
No comments:
Post a Comment