Kikosi cha Yanga kikifanya mazoezi nchini Uturuki leo.
Na Baraka Kiziguto, Uturuki
Timu ya
Young Africans Sports Club yenye makao makuu yake jijini Dar es salaam
nchini Tanzania siku ya jumamosi itashuka dimbani kucheza mchezo wa kirafiki na
timu ya Arminia Bielefeld ya kutoka nchini Ujerumani, mchezo utakaofanyika
katika mji wa Antalya.
Young
Africans ambayo imeweka kambi ya mafunzo jijini Antalya itatumia mchezo huo
kama fursa pekee ya kuweza kujipima uwezo dhidi ya timu hiyo ya Ujerumani
ambayo pia imekuja kambi y amafunzo kujiandaa na mzunguko wa ligi daraja la
pili nchini Ujerumani.
Kocha
Mkuu wa Young Africans Ernest Brandts amesema kwao ni furaha kwa kupata nafasi
ya kucheza na timu kubwa kama ya Armini Bielefeld ambayo inawachezaji wa
kiwango cha kimataifa hivyo anaamini utakua ni mchezo safi na kuwavutia.
"Unajua
tuna siku sita (5) tangu tufike hapa mjini Antalya Uturuki na tumeshafanya
mazoezi kwa siku nne (4) hivo fursa ya kupata mchezo wa kirafiki ni nzuri
sana kwetu kwani itanipa nafasi ya kuona wachezaji wangu wameshayashika kwa kiasi
gani mafunzo yangu alisema 'Brandts'
Arminia
Bielefeld imeshawasili mjini Antalya kwa ajili ya kambi yake ya mafunzo
na hivyo kwao pia ni fursa nzuri ya kuweza kujipima uwezo na timu ya Young
Africans ambao ni mabingwa mara 23 katika ligi kuu ya Tanzania.
Leo
asubuhi Young Africans imeendelea na mazoezi katika viwanja wa Fame Residecne
tayari kabisa kujiandaa na mchezo huo utakaochezwa siku ya jumamosi mjini
Antalya.
Kikosi
cha wachezaji 27 waliopo mjini Antalya wote wako katika hali nzuri na hakuna
maheruhi hata mmoja hali itakayompa kocha Brandts kuamua kumtumia mchezaji
yoyote katika mchezo huo.
Picha hizi ni kwa hisani ya www.youngafricans.co.tz
No comments:
Post a Comment