Msemaji wa Chadema, Tumaini Makene wa pili kutoka kushoto, akifafanua jambo linalohusu chama chao.
Na Kambi Mbwana, Dar es Salaam
CHAMA Cha Demokrasia na Maendeleo Chadema kimetangaza
kuwachunguza na kuwapa ushauri wapenzi wao wanaoamua kufungua blogs na kuziita
jina la (Chadema Blog), ili wajiendeshe bila kukiathiri chama chao.
Hayo yamesemwa na Msemaji wa Chadema, Tumaini Makene,
alipokuwa akizungumza na Handeni Kwetu jana, kufuatia habari za baadhi ya blogs
zinazojiita Chadema, taarifa zao kupingana kutokana na kuchukua stori kwenye
baadhi ya magazeti.
Makene alisema sio blogs zote zinatumiwa na kuangaliwa na Chadema,
hivyo ili wapenzi wao wajiendeshe vizuri, wataanza kuwapa somo, ikiwamo
kuwazuia kuchukua stori zinazoandikwa katika magazeti mbalimbali nchini.
Alisema hawawezi kuwazuia watu hao, maana wanafanya hivyo
kwa mapenzi ya kueneza sera za chama chao, lakini wakati mwingine wanashindwa
kuelewa mbinu za kuandikwa habari hata zile ambazo zinalengo la kuhujumu chama
chao.
Zimekuwapo blogs nyingi kama njia ya kupeana habari kwa
mtandao, hivyo sisi Chadema tunashukuru kwanza kwa kupata Watanzania wengi
wanaona kuwa wakifanya hivyo wataonyesha mapenzi yao kwa chama chetu hapa
Tanzania.
Kwa sababu hiyo, tutakachofanya ni kuwaelimisha na kuwaambia
kuwa sio kila habari inayotoka kwenye gazeti ni nzuri kwa Chadema, ukizingatia
kuwa katika siasa kuna mbinu nyingi zinazotumiwa na vyama, hivyo hili
litawasaidia kwa kiasi kikubwa,” alisema Makene.
Kwa mujibu wa Makene, habari zinazoandkwa na baadhi ya
magazeti wakati mwingine ni za kupishana kiasi ambacho kinaweza kuwafanya
wapenzi na wanachama wao washindwe kuelewa, ingawa aliwapongeza watu wote wenye
mapenzi mema na Chadema hadi kufiia kuanzisha blogs kwa ajili ya kueneza elimu
ya chama chao.
No comments:
Post a Comment