Mbunge wa Korogwe vijijini, Profesa Maji Marefu
Na Mwandishi Wetu, Tanga.
MBUNGE wa Korogwe vijijini kwa tiketi ya Chama Cha
Mapinduzi (CCM), Steven Ngonyani (Maji Marefu), amemwagiwa sifa na Mwenyekiti
wa Chama Cha United Demokratic Party (UDP) Mkoa wa Tanga, Mhina Peter.
Peter amesema Maji Marefu anastahili heshima kutokana na
kuchapa kazi bila kuchoka huku akiwa karibu na wananchi wake, hivyo ni mbunge
bora kwa upande wake.
Akizungumza leo asubuhi mkoani Tanga, Peter alisema mbali
na kuwa karibu na wananchi, pia anatekeleza ahadi zake kwa wakati.
“Kwa maoni yangu Maji Marefu anastahili kuwa bora na huyu
ndio mbunge wangu bora kwa mwaka ulioisha, maana amekuwa akishiriki katika
juhudi za maendeleo kwa wananchi wake,” alisema.
No comments:
Post a Comment