Marehemu Sajuki
Na Kambi
Mbwana, Dar es Salaam
MSANII wa
filamu hapa nchini, Juma Kilowoko, maarufu kwa jina la Sajuki, amefariki Dunia
leo saa moja asubuhi katika Hospitali ya Taifa Muhimbili.
Sajuki
amekufa huku akiwa na kumbukumbu za kuanguka mwishoni mwa mwezi Desemba mkoani
Arusha, alipokwenda kufanya shoo, akiizungumzia kama kujichanganya kwa ajili ya
kutafuta fedha za kumpeleka tena India kupata matibabu.
Mke wa marehemu Sajuki, (Wastara)
Akizungumza
mapema leo, Katibu wa Baraza la Filamu Tanzania (TAFF), Wilson Makubi, alisema
kwamba maandalizi ya msiba huo yatatangazwa baada ya wahusika na wadau
kujipanga.
Alisema
habari za kifo chake zimeanza kusambaa tangu saa moja asubuhi, hivyo wadau na
mashabiki wake watapewa utaratibu juu ya msiba wa msanii huyo mwenye mafanikio
katiika tasnia ya filamu Tanzania.
“Sajuiki
ni msanii mahiri na amekufa katika siku ya pili ya mwaka huu mwezi Januari,
hivyo hakika ni pengo kwa wasanii wote pamoja na mashabiki kwa ujumla,
ukizingatia kuwa tulikuwa na mapenzi naye.
“Watu
walishajichanga kwa ajili ya kumpeleka India msanii huyo jambo ambalo
lilifanikiwa kwa dhati, hata hivyo jitihada hizo Mungu ameona amchukuwe kiumbe
wake kwa ajili ya maisha ya milele,” alisema.
Kifo cha
Sajuki kwa wasanii kimefungua dimba kwa mwaka 2013, huku ukiwa na kumbukumbu za
kuondokewa na wasanii watano katika kipindi cha mwaka 2012, akiwamo Steven
Kanumba, Sharomillionea na wengineo.
No comments:
Post a Comment