Waziri
Mkuu wa zamani na mbunge wa Jimbo la Monduli, Edward Lowassa, akitoa hotuba kwa
wananchi wa kijiji cha Mswakini, Wilayani Monduli, wakati wa uzinduzi wa Vikoba
kijijini hapo.
Wakati
Waziri Mkuu wa zamani, Edward Lowassa, ambaye pia ni mbunge wa Monduli mambo
yalionekana hivi, akiwa anaingia sambamba na mke wake, Regina Lowassa, katika
uzinduzi wa Vikoba katika kijiji cha Mswaki mapema leo.
Afisa
Maendeleo ya Jamii Wilaya ya Monduli, aliyejulikana kwa jina laa Judith, akikabidhi
hati kwa Edward Lowassa, ikiwa ni ishara ya uzinduzi wa Vikoba katika kijiji
cha Mswakini
Na
Mwandishi Wetu, Monduli
WAZIRI
Mkuu wa zamani, ambaye pia ni Mbunge wa Monduli, Edward Lowassa, amesema kuwa
ushirika wa Vikoba ni sawa na mshipa wa damu kwa sera ya maisha bora kwa kila
Mtanzania.
Lowassa
ameyasema hayo leo katika uzinduzi wa Vikoba vya Mswakini, wilayani Monduli,
ikiwa ni ishara ya kutambua njia ya kumkomboa Mtanzania.
Akizungumza
na wanakikundi hicho, Lowassa alisema kwamba hiyo ni sera aliyoingia nayo
madarakani Rais Jakaya Kikwete.
Alisema
kuna haja ya kuwa na vikoba nchi nzima kwa ajili ya kuongeza kasi ya maisha
bora kwa kila Mtanzania, ukizingatia ni mfumo mzuri kiutendaji wa biashara kwa
wote waliokuwa kwenye vikundi hivyo.
No comments:
Post a Comment