Wastara akiwa amefunikwa uso huku akilia kwa uchungu |
Na Kambi Mbwana, Dar es Salaam
NI
dhahiri kuwa wakati mwingine baadhi ya watu hutabiri vifo vyao, kiasi hata ha
kuwazuia ndugu zao waache kufuja fedha katika kuuguza kutokana na maradhi yao.
Rais wa TAFF, Simon Mwakifambwa, akitangaza kamati za kuratibu msiba wa Sajuki, nyumbani kwake Tabata Bima leo.
Hii
hutokea sana katikaa jamii. Baadhi yao hufikia kusema “Nasikitika siwezi tena
kuishi katika Dunia hii. Mwisho wa maisha yangu"
Nimelazimika
kuandika maneno haya, maana kauli ya mwisho ya msanii wa filamu, Juma Kilowoko,
maarufu kama Sajuki ilikuwa ni kumtaka mke wake amuombee msamaha kwa watu wote
aliowahi kuwakosea katika kipindi cha maisha yake.
Maneno
haya yalikuwa mahungu kwa mwanadada Wastara Juma, mke wa marehemu Sajuki.
Naomba uwaambie ndugu zangu kuwa uhai wangu tena ni mdogo sana.
Siwezi
kuishi, maana sioni dalili nzuri za kuniponya” maneno haya yalitoka katika
kinywa ha Wastara ambaye kwa kipindi hicho, alikuwa akilia na kusaga meno
kuonyesha huzuni yake.
Jamani
mimi nitaweza kuishi peke yangu? Sajuki wangu kwanini umenitendea hivyo? Yani
kweli unasema nikuagie kwa watu kama hutapona kumbe kweli umeshajua unaniacha
peke yangu,” Wastara aliendelea kulalama, huku akizidi kufunikwa uso wake.
Inauma
sana. Sajuki amekufa katika kipindi ambacho watu wengi walifahamu uhai wake
utaendelea kuwapo. Kama Sajuki alistahili kufa, basi ingekuwa mwaka jana
alipokuwa kwenye hali mbaya kiasi cha kulazimika kuchangiwa na wasamalia wema
kwa ajili ya kwenda India.
Kwa
mujibu wa taarifa, Sajuki alipokwenda India, maradhi yaliyompeleka ya Tumbo
yaliongezeka mengine ya Kansa ya ngozi. Shughuli ilikuwa kubwa sana. Mbaya
zaidi, Sajuki hakuwa na uwezo wa kustahimili ugonjwa wake.
Hata
hivyo, katika kipindi cha mwisho wa mwaka 2012, Sajuki alikuwa kwenye afya
kiasi Fulani. Muda wote alikuwa akisikika akimshukuru Mungu wake kwa kumpa
uhai.
Katika
kumshukuru Mungu, Sajuki pia alikuwa haishi kumshukuru Mungu kwa kumpa mke
mwema, mwenye upendo wa kweli. Mwanamke ambaye licha ya kukutana na vikwazo
vingi, lakini aliendelea kufunga khanga yake akitetea upendo wake kwa Sajuki.
Kwanini?
Pamoja na yote hayo, lakini leo tunaongelea kifo chake. Na saa tano za asubuhi,
keshokutwa Ijumaa, mwili wake utazikwa katika makaburi ya Kisutu, jijini Dar es
Salaam.
Msiba
wake ni mzito sana. Wasanii wote pamoja na wadau wanalia. Serikali nayo kwa
kupitia Waziri wa Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo inalia kutokana na msiba
wa Sajuki.
Amekufa
na katika kipindi ambacho watu wanashangaa kwanini bundi wa vifo vya wasanii wa
maigizo na filamu anaendelea kukaa kwenye paa za nyumba za wasanii hao
Tanzania?
Sajuki
amekufa katika kipindi cha siku 37 kabla ya arobaini ya msanii Hussein Mkiety,
maarufu kama Sharomillionea, inayotarajiwa kusomwa Januari nne, kijijini kwao
Lusanga.
Mamia ya
watu walikuwa wakimiminika katika viwanja vilivyokuwapo nyumba ya marehemu
Sajuki, maeneo ya Tabata Bima. Ukifika hapo nyuso zao zinasema.
Wengi
wanalia na kuomboleza kifo hicho. Shirikisho la Filamu Tanzania (TAFF), kwa
kupitia Rais wake, Simon Mwakifambwa na wadau wengine wamekuwa wakipita huku na
kule kwa ajili ya kuweka sawa taratibu za msiba huo wa Sajuki.
Taarifa ya Waziri wa Habari, Vijana,
Utamaduni na Michezo Dkt. Fenella
Mukangara amewatumia salamu za rambirambi, ndugu, jamaa na
wasanii wote nchini kufuatia kifo cha Sajuki ilimuumiza na kutaka Watanzania
kumuombea dua njema.
Kwa mujibu wa taarifa hiyo kifo chake ni
pengo kubwa kwa Serikali, wadau wa tasnia ya filamu na michezo ya kuigiza
nchini kwa ujumla. “Nimepokea kwa masikitiko makubwa taarifa
ya kifo cha Sajuki na sina maneno ya kuelezea masikitiko na huzuni nilinayo,
kwani kifo chake ni pigo katika tasnia ya filamu za michezo ya kuigiza,”
alisema Dkt. Mukangara.
Dkt. Mukungara amewataka ndugu, jamii na
wasanii wote kuwa wavumilivu na watumilivu wakati wote wa msiba na kumuombea
marehemu makao mema kwa Mwenyezi Mungu. Sajuki ni mzaliwa wa mkoa wa Ruvuma na
sanaa yake alianza kujihusisha nayo alipojiunga na kikundi cha Kaole Sanaa
Group, ambapo baadaye alicheza filamu Revenge ya Kampuni ya RJ.
Mwaka 2008 aliamua kuanza kutengeneza
kazi zake mwenyewe ambapo filamu yake ya kwanza iitwayo Two Brothers kwa
kushirikiana na Shija Deogratious ilitoka. Sajuki baadaye aliamua kuanzisha kampuni
yake iitwayo WAJEY Production Company ambapo alitengeneza filamu nyingi
zikiwemo Mboni Yangu, Round, Briefcase , Kijacho, Kozopata, Mchanga na Keni,
077( Zero Seven Seven).nk
Sajuki alifanikiwa kucheza michezo ya kuigiza na filamu na wasanii wengi wenye
majina hapa nchini. Sajuki amebobea katika Uigizaji, Utayarishaji na Uongozaji
wa filamu. Sajuki alianza kuugua mwaka 2010 na hali
ilizidi kudhoofu mwaka 2011, ambapo alikwenda kutibiwa nchini India kutokana na
michango kutoka kwa wadau tasnia ya filamu.
Alirudi na kuonekana kapata nafuu kidogo
jambo ambalo lilileta matumaini na furaha kwa watanzania; aliporejea tu aliweza
kutoa filamu iitwayo Kivuli huku filamu nyingine ikiwa katika hatua ya
utengenezaji.
Ambapo
pia filamu ya kumchangia iliandaliwa na kuitwa Sayla na kushirikisha wasanii na
viongozi wa serikali, akiwamo Zitto Kabwe, ambaye ni Mbunge wa Kigoma
Kaskazini, January Makamba na wengineo.
No comments:
Post a Comment