Na Baraka Kizuguto, Uturuki
MABINGWA
wa zamani wa Tanzania Bara, Yanga SC, kesho inajitupa katika Uwanja wa Selen
Football kwa ajili ya kupepetana na timu ya Denizlisport ya nchini Uturuki.
Taarifa
iliyotumwa na kutoka Uturuki zinasema Yanga iliyoweka kambi ya mafunzo jijini
Antalya, nchini Uturuki, itatumia mchezo huo kama njia ya kujipima nguvu na
timu hiyo la Denizlispor FC iliyoshuka daraja, ikitokea ligi kuu ya nchi hiyo.
Kocha wa
Yanga, Ernest Brandts, pichani, amesema kupata mechi kubwa kama hiyo ni nafasi ya
kucheza na timu kubwa kama ya Denizlispor FC yenye wachezaji wa kiwango cha
kimataifa.
Alisema baada
ya kuwa na wiki moja ya mazoezi na mechi moja ya kirafiki dhidi ya Armini
Bielefeld ya Ujerumani mwishoni mwa wiki, itakuwa ni fursa nyingine ya kucheza
mchezo mwingine kwa ajili ya kujiweka sawa zaidi.
No comments:
Post a Comment