Licha ya
ufukwe kuwa sehemu ya starehe kwa watu wengi, lakini baadhi ya wazazi
wameshindwa kuwa makini kiasi cha kuwaachia watoto kuogelea bila kuangalia
usalama wao. Pichani mtoto huyu aliyembeba mwenzake akionekana akikimbia wimbi
la maji katika ufukwe wa Bahari ya Hindi, Coco Beach, baada ya kuangushwa kiasi cha kujiweka hatarini na aliyembeba. Picha na
Kambi Mbwana.
Watanzania
wanaoishi jijini Dar es Salaam, wakijimwaga
katika ufukwe wa bahari ya Hindi, Coco
Beach, leo wakisherehekea
Sikukuu ya Mwaka Mpya. Ufukwe huo ulijaa watu wengi waliokwenda kutembelea
katika eneo hilo
wao na familia zao. Hata hivyo, watoto walikuwa wengi wakiingia baharini bila
kuwa na waangalizi jambo linaloweza kuwa hatari kwao. Picha na Kambi Mbwana.
No comments:
Post a Comment