Naibu Waziri wa Kazi na Ajira, Dkt. Makongoro Mahanga, akizungumza msibani jioni ya leo, Tabata Bima. Kulia kwake ni Steve Nyerere wakati mwenye suti nyeusi ni Idd Azzan anayeuguza mkono wake.
Na Kambi
Mbwana, Dar es Salaam
NAIBU
Waziri wa Kazi na Ajira ambaye pia ni mbunge wa Segerea, Dkt. Makongoro
Mahanga, ametoa laki mbili kama rambirambi yake katika msiba wa msanii Juma
Kilowoko, Sajuki, nyumbani kwake Tabata Bima, leo jioni.
Kitale rais wa mateja kushoto akiranda randa katika msiba wa Sajuki leo.
Mbali na
Mahanga, wengine waliotoa rambirambi zao leo ni pamoja na Mbunge wa Kinondoni,
Idd Azzan, aliyetoa laki tano, Naibu Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM),
Mwigulu Nchemba, aliyetoa Sh 1,000,000, Meya wa Ilala, Jery Slaa aliyetoa Sh
1,000,000, katika msiba unaohitaji fedha zisizopungua milioni nane.
Msanii Dokii kushoto, akisikiliza maongezi ya mbunge wa Kinondoni, Idd Azzan katikati na msanii Masanja Mkandamizaji mwenye miwani, A.K.A Nikikukera, livumini aloniiiiiiii.
Katika
maneno yake kwa waombolezaji, Mahanga aliwataka Watanzania kumuombea Sajuki
kutokana na msiba wake kuwa pigo kubwa katika tasnia ya sanaa sanaa hapa
nchini.
Alisema
kifo cha Sajuki ni pigo, hivyo akiwa kama Mtanzania, Mbunge wa alipofia msanii
huyo, ameumia vikali na kuahidi kuwa karibu na wote kwenye msiba huo.
“Nimeumia
kupita kiasi na hakika msiba huu umekuja katika kipindi ambacho ni kigumu mno kwetu,
hivyo naahidi kuwa karibu katika shughuli hizi za kumhifadhi kijana mwenzetu,
Sajuki,” alisema.
Azzan
yeye alitumia muda mwingi kumuombea dua njema Sajuki, huku akisema anashukuru
kuona msanii huyo ni mwenye kujua shukrani, hasa alipowashukuru Watanzania kwa
kumchangia.
Wengine
waliotoa rambirambi hizo ni pamoja na Mkurugenzi wa Utafiti na Matukio wa
Clouds Media Group, Ruge Mutahaba, aliyetoa Sh laki tano, huku msanii Steve
Nyerere, akiwashukuru wote kwa michango yao na kusema hadi sasa wamebakiwa na
pengo la Sh milioni tatu.
“Tuna
pengo la Milioni tatu baada ya wadau wote kutoa na kufikia Sh 5,000,000 ambapo
kwakweli wakati tunaendelea kuwaomba wenzetu, waliotoa wote tunawashukuru kwa
kushiriki kuwa na sisi,” alisema.
Watu
wengi walikutwa katika nyumba ya marehemu Sajuki kwa ajili ya kuomboleza msiba
huo kwa ajili ya mpendwa wao anayezikwa kesho saa tano asubuhi, katika makaburi
ya Kisutu, jijini Dar es Salaam.
No comments:
Post a Comment