Yanga wakiwa mazoezini nchini Uturuki
Na Baraka Kizuguto, Uturuki
Timu ya Yanga kesho itashuka dimbani kucheza mchezo wa
kirafiki na timu ya Arminia Bielefeld ya Ujerumani katika mchezo utakaofanyika
mjini Antalya, nchini Uturuki, kuanzia saa 10 za jioni kwa saa za Afrika
Mashariki na Kati.
Yanga imeweka kambi ya mafunzo katika mji wa Antalya huku
ikifanya mazoezi tangu siku ya jumatatu na wachezaji wote wameonekana kufurahia
mazingira ya kambi na huduma zote kwa ujumla.
Baada ya kufanya mazoezi kwa takribani siku tano (5)
mfiululizo itatumia mchezo wa kesho dhidi ya timu ya Arminia Bielefed kama
kipimo tosha cha maendeleo ya mafunzo yanayoendelea nchini Uuturuki.
Kocha wa timu hiyo, Mholanzi, Ernie Brandts, amesema
anashukuru wachezaji wake wapo vizuri kwa ajili ya mchezo huo wa kesho.
Aidha Brandst alisema anajua mchezo wa kesho utakua mgumu
kwakuwa Arminia Bielefeld ni timu nzuri na imekuwa ikishiriki Ligi Kuu ya
Ujerumani mara kadhaa.
No comments:
Post a Comment