Sajuki enzi za uhai wake akiwa na mke wake, kipenzi chake, Wastara
Na Mwandishi Wetu, Dar es Salaam
WADAU wa sanaa hapa nchini, wameendelea kummwagia sifa
mwanadada Wastara Juma, aliyekuwa mke wa marehemu Sadiki Juma Kilowoko, maarufu
kama Sajuki kuwa ana moyo wa aina yake.
Hiyo imetokana na historia ya uhusiano wake na Sajuki hadi
kufunga ndoa kukumbwa na mitihan mingi, jambo ambaloh hivyo halikumfanya ajiweke
kando na Sajuki.
Akizungumza na Handeni Kwetu, Mbunge wa Kigoma Kaskazini,
kwa tiketi ya Chadema, Zitto Kabwe, alisema kwamba Wastara ana mapenzi ya dhati
na anastahili sifa.
Alisema ameweza kumuuguza mumewe mwanzo hadi mwisho wa uhai
wake, jambo ambalo limekuwa gumu kwa baadhi ya watu, kadri muda unavyozidi
kwenda mbele.
"Ni mfano wa kuigwa kwakweli kutokana na historian a matatizo
mengi yaliyowakumba yeye na mumewe hadi kufariki na kuzikwa Ijumaa katika
makaburi ya Kisutu," alisema.
Naye Mbunge wa Kinondoni, kwa tiketi ya (CCM), Idd Azzan,
alisema amekuwa karibu na sanaa kiasi cha kumuona Wastara ni miongoni mwa
wanawake makini.
"Kwa dunia ya leo kumuuguza mume wako katika kipindi kigumu
cha ugonjwa wake, hadi kuchangiwa fedha za kumpeleka India, hakika baadhi yao
wanaweza kuleta wasiwasi kidogo,” alisema Azzan.
Azzan ni miongoni mwa wabunge wanaofuatilia sanaa kwa karibu
zaidi, huku wasanii wengi wakikimbilia kwake kila wanapokuwa na jambo
linalohusu msaada kutoka kwa jamii nzima.
No comments:
Post a Comment