Rais Jakaya Kikwete akitia mchanga kaburini.
Na
Kambi Mbwana, Dar es Salaam
RAIS
wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Jakaya Mrisho Kikwete, leo ameongoza mamia ya waombolezaji katika
mazishi ya msanii Juma Kilowoko, maarufu kama Sajuki, katika makaburi ya
Kisutu, jijini Dar es Salaam, yaliyofanyika saa saba za mchana.
Baba wa marehemu, mzee Juma Kitilu.
Mbali
na Kikwete, wengine walioshiriki kwenye mazishi hayo ni pamoja na Zitto Kabwe,
ambaye pia ni Mbunge wa Kigoma Kaskazini, Idd Azzan, Mbunge wa Kinondoni na Said
Mtanda, Mbunge wa Mchinga, sanjari na wasanii na wanamichezo, akiwamo mlinda
mlango wa Simba, Juma Kaseja.
Katika
mazishi hayo, ambayo hata hivyo Kikwete hajaongea lolote, alionekana kufuatilia
zaidi tukio hilo la mazishi ya Sajuki, aliyefariki Dunia juzi, katika Hospitali
ya Taifa, Muhimbili.
Msanii Profesa Jay wa tatu kutoka kulia.
Awali
katika maandalizi ya mwili wa Sajuki katika makaburi hayo, wadau waliojipanga
kuanzia lango la kuingilia, walijikuta wakipigwa chenga na jeneza la msanii
huyo lililoingizwa kwa kupitia geti ka nyuma na kuibua mkanyagano mkubwa kutoka
kwa wadau wa filamu waliokwenda kuzika.
Kama
ilivyokuwa kawaida ya wasanii kuwa na mvuto na misiba yao kugonga hisia za watu
wengi, kuanzia nyumbani hadi makaburini, watu wengi walijitokeza, wakiwamo
baadhi ya akina dada waliojipanga kando ya barabara inayoingia katika makaburi
hayo.
Jeneza la Sajuki likishushwa kwenye gari.
Awali
marehemu Sajuki alipangwa kuzikwa saa tano za asubuhi, lakini ratiba
ilibadilishwa na kuzikwa saa saba baada ya swala ya Ijumaa. Mazishi ya Sajuki
yalivuta watu na kuwapa majonzi makubwa.
Wasanii
wengi walijitokeza kuanzia nyumbani hadi makaburini kwa ajili ya kushiriki
mazishi ya msanii huyo ambaye pia amesababisha arobaini ya mchekeshaji maarufu,
Hussein Mkiety, Sharomillionea kusitishwa jana na kupangwa kufanyika leo
kijijini kwao Lusanga.
Mara
baada ya gari lililobeba mwili wa marehemu Sajuki kufika makaburini hapo,
mkanyagano ulizidi kuwa mkubwa, hasa baada ya mashabiki kuvamia wakitaka
kuubeba mwili huo na kuusindikiza katika nyumba yake ya milele.
Hata
hivyo, waliokuwa kwenye jukumu la mipango ya mazishi, walielekea kufanikiwa
kuwadhibiti watu hao wenye mapenzi mema na Sajuki, ingawa baadaye hali ilikuwa
tofauti kidogo pale msukuamano ulipoibuka kila mmoja akitaka kukaa karibu na
kaburi.
Hali
hiyo ilisababisha malalamiko kutoka kwa waandishi waliokuwa wakichukua tukio
hilo kwa ajili ya kuwahabarisha wadau na mashabiki wa sanaa wa Tanzania, juu ya
safari ya mwisho ya msanii Sajuki, aliyefariki Dunia juzi.
Sajuki
aliyeacha mke na mtoto mmoja, amefariki juzi katika Hospitali ya Taifa ya
Muhimbili, huku akifanikiwa kuzikwa na watu mbalimbali, akiwamo rais, wabunge
na wasanii wengine maarufu wanaotamba hapa nchini.
Viongozi
ambao nao wameshiriki msiba huo ni pamoja na Mwigulu Nchemba, Naibu Katibu Mkuu
wa Chama ha Mapinduzi (CCM), Halima Mdee, Mbunge wa Kawe, Ester Bulaya, Mbunge
wa Viti Maalumu, Junuary Makamba, Mbunge wa Bumbuli ambaye pia ni Naibu Waziri
wa Mawasiliano, Sayansi na Teknolojia na Naibu Waziri wa Kazi na Ajira, Dkt.
Makongoro Mahanga na wengineo.
Marehemu
Sajuki alizaliwa mwaka 1986 Songea alipopata elimu ya msingi na sekondari,
kabla ya kuhamia jijini Dar es Salaam na kujiunga moja kwa moja katika kundi la
Kaole Sanaa Group na kuingia kwenye mchakato wa kutafuta jina kwenye tasnia
hiyo.
No comments:
Post a Comment