Dada huyu akishuka kwenye gari huku analia
Na Kambi Mbwana, Dar es Salaam
MSANII wa Vichekesho hapa nchini, Hamis Changale, maarufu
kama Mtanga, ameshangazwa na kadi nyekundu zinazoendelea kwa wasanii na
kusababisha vifo vyao, hali inayoogopesha.
Wadau na wasanii wakijadili jambo kwenye msiba wa Sajuki
Mtanga aliyasema hayo mapema leo, akisema kadi hizo nyekundu
zinatolewa kwa wasanii nyota, akiwamo Steven Kanumba, Sharomillionea, Mropelo,
John Maganga na sasa ameondoka Juma Kilowoko, maarufu kama Sajuki.
Thea akijadili jambo msibani kwa Sajuki
Mtanga alisema vifo hivyo ni kama kadi nyekundu kwa wasanii
Tanzania, jambo linalomnyima raha kwa kusikia au kuona nyota wanaendelea
kupukutika kila siku kwa sababu za kushangaza.
Hali inavyoendelea msiba wa Sajuki Tabata Bima
“Alipokufa Kanumba, watu wengi tuliogopa kutokana na kifo
chake, lakini bado ikaja tena kwa wasanii zaidi ya watano, akiwamo Sharomillionea
aliyekufa mwishoni mwa mwaka jana na kuzikwa kwao Lusanga.
Msanii wa vichekesho, Mtanga
“Na leo tena mwenzetu Sajuki anafungua pazia la vifom kwa
wasanii wa Tanzxasnia kwa mwaka huu kuonyesha kuwa bado Mungu anaendelea kutoa
kadi nyekundu kwa wasanii kila siku ya Mungu,” alisema Mtanga.
Sajuki enzi za uhai, wakati ni mgonjwa akiwa na mke wake, Wastara
Kwa mujibu wa Mtanga, kadi nyekundu katika mchezo wa soka ni
tukio linalotokea kati ya mchezaji uwanjani na mwamuzi kwa ajili ya kumtoa nje
ya uwanja mchezaji aliyefanya kitendo ambacho si cha kiungwana.
Taarifa za kifo cha Sajuki kimeendelea kuwagusa Watanzania
na viongozi wa Serikali, baada ya Naibu Waziri wa Mawasiliano, Sayansi na
Teknolojia, January Makamba kuwa miongoni mwa waombolezaji waliofika msibani
Tabata Bima kwa ajili ya kuungana katika msiba wa Sajuki.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Jakaya Mrisho
Kikwete, aliwata Watanzania kutumia fursa ya kifo kwa ajili ya kumuombea
marehemu pamoja na kuwataka wasanii wawe kitu kimoja.
No comments:
Post a Comment