Kocha wa Stars, Kim Poulsen
Na Kambi Mbwana, Dar es Salaam
WACHEZAJI 22 wameteuliwa na kocha
Mkuu wa timu ya Taifa (Taifa Stars), Kim Poulsen kwa ajili ya kuingia kambini
Januari 6 mwaka huu jijini Dar es Salaam kwa kujiandaa na mechi za kirafiki dhidi
ya Morocco
itakayochezwa Machi mwaka huu.
Kwa mujibu wa Kocha Kim, wachezaji hao wanatakiwa kuripoti kambini
katika hoteli ya Tansoma saa 11.30 jioni tayari kwa mazoezi yatakayoanza
Januari 7 mwaka huu.
Wachezaji walioitwa ni makipa Juma
Kaseja kutoka Simba ambaye pia ndiye nahodha wa Stars, Aishi Manula na Mwadini
Ally wote kutoka Azam. Mabeki ni Aggrey Morris (Azam), Amir Maftah (Simba),
Erasto Nyoni (Azam), Issa Rashid (Mtibwa Sugar), Kelvin Yondani (Yanga), Nadir
Haroub (Yanga) na Shomari Kapombe (Simba).
Viungo ni Salum Abubakar (Azam),
Athuman Idd (Yanga), Amri Kiemba (Simba), Khamis Mcha (Azam), Frank Domayo
(Yanga), Mwinyi Kazimoto (Simba) na Shabani Nditi (Mtibwa Sugar).
Washambuliaji ni John Bocco
(Azam), Mbwana Samata (TP Mazembe, Jamhuri ya Kidemokrasi ya Congo- DRC),
Mrisho Ngasa (Simba), Simon Msuva (Yanga), na Thomas Ulimwengu wa TP Mazembe,
Jamhuri ya Kidemokrasi ya Congo (DRC).
Mbali ya Kim, benchi la ufundi la
Taifa Stars linaundwa na Sylvester Marsh (Kocha Msaidizi), Juma Pondamali
(Kocha wa makipa), Leopold Tasso (Meneja), Dk. Mwanandi Mwankemwa (Daktari wa
timu), Frank Mhonda (Mtaalamu wa tibamaungo) na Alfred Chimela (Mtunza vifaa).
No comments:
Post a Comment