https://tpc.googlesyndication.com/simgad/8045142562622600543


Recent Post

Sunday, January 06, 2013

Wananchi Handeni wahofia kutokea machafuko


Mbunge wa Handeni, Abdallah Kigoda
 
Na Mashaka Mhando, Handeni
WANANCHI wilayani Handeni, wameingia hofu huenda kutatokea machafuko baina ya wakulima na wafugaji kutokana na kukithiri kwa vitendo vya wafugaji kuingiza mifugo yao kwenye mashamba ya wakulima na kisha kesi za migogoro hiyo kumalizwa huku wafugaji wakishinda katika vyombo vya dola.

Wakizungumza kwa nyakati tofauti, wakimweleza Mbunge wa jimbo hilo Dkt Abdallah Kigoda anayetembelea jimbo lake kuhamasisha maendeleo na kukagua miradi mbalimbali, wananchi hao walisema kuwa hofu ya kutokea mapigano ni kubwa.

"Mheshimiwa mbunge, kusema kweli tunasikitika hapa kijijini ndugu zetu wamang'ati wamekuwa wakiingiza mifugo yao kwenye mashamba yetu na kula mazao lakini tunapokwenda kwa viongozi wa kijiji na hata kesi kwenda mahakamani basi wafugaji wanapata haki, sasa mheshimiwa mbunge, ukija kusikia tumepigana ni kwasababu hatuna msaada," alisema Shakili Adam mkazi wa kijiji cha Kilimamzinga.

Akizungumza katika mikutano ya hadhara katika kata za Magamba, Kang'ata na Kwamatuku Mbunge wa jimbo hilo, Dkt Kigoda alikiri kupata malalamiko kila vijiji alivyovitembelea kuhusu migogoro ya wakulima na wafugaji hatua ambayo ametupa lawama kwa viongozi waliowapokea wafugaji hao bila utaratibu na sasa kutishia usalama wa wananchi wa wilaya hiyo.

Alisema alipata malalamiko haya katika kata ya Kwamsisi kwamba viongozi wa kijiji wamewapokea wafuaji hao lakini hali ilivyo viongozi wa kata lazima waliangalie kwa kina ili kuwe na kuheshimiana baina ya wafugaji na wakulima.

"Tatizo la wafugaji sasa Handeni ni kero, malalamiko haya yametokea kila eneo, wafugaji wanalishia mazao na wao wakiulizwa wanasema mifugo yao inathamani kuliko mazao hayo,” alisema Dkt Kigoda.

Dkt Kigoda ambaye ni Waziri wa Viwanda na Biashara alidai wana wasiwasi kwamba wafugaji wamekuwa wakitoa rushwa kwasababu haiwezekani kesi ya mfugaji na mkulima inapopelekwa mahakamani hata kama mkulima mazao yake yameliwa na ng'ombe lakini mfugaji ndiye anayepata haki na kushinda kesi.

"Sisi Handeni siyo kwamba tunawakataa wafugaji hawa hapana tunaomba tueleweke kwamba wilaya hii ni ya wakulima na wafugaji lakini hawa walioingia hivi karibuni wanataka kuleta machafuko ambayo kama viongozi hatuwezi kukubali kutokea mapigano na kabla hayajatokea basi tuwarudishe walipotoka," alisema Dkt Kigoda na kuongeza;

No comments:

LinkWithin

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...