R.I.P Sajuki
Msanii wa filamu, Jini Kabula akiwa kwenye msiba wa marehemu Sajuki, maeneo ya Tabata Bima jana
Na
Mwandishi Wetu, Dar es Salaam
LEO
saa tano za asubuhi, mwili wa msanii maarufu nchini, Juma Kilowoko, Sajuki
unazikwa katika makaburi ya Kisutu, jijini Dar es Salaam kuashiria kuwa ni
kweli mwisho wa uhai wa kijana huyo umefika.
Msanii Tuesday Kihangala akiwa msibani kwa Sajuki
Sajuki
alifariki juzi katika Hospitali ya Taifa Muhimbili na kuhuzunisha wengi,
wakiwamo wasanii, mashabiki na serikali kwa ujumla kutokana na ubora wake
kwenye sanaa.
Taratibu
za mazishi za Sajuki zimeshakamilika huku kamati mbalimbali za kuratibu
shughuli hiyo zikifanywa kwa umakini mkubwa.
Eneo
la nyumba ya Sajuki, Tabata Bima, mashabiki wengi walijitokeza kuomboleza msiba
wa msanii huyo aliyeuigua kwa muda mrefu kabla ya kifo chake.
Awali,
ilitarajiwa kuwa Sajuki angezikwa kwao Songea, lakini wasanii waliomba familia
ya Sajuki ili Watanzania wanaoishi jijini Dar es Salaam washiriki kwa karibu
kwakuwa ndipo alipoishi marehemu kwa muda mrefu.
Serikali
kwa kupitia Waziri wa Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo, Dkt. Fenella
Mukangara, Naibu Waziri wa Mawasiliano, Sayansi na Teknolojia, January Makamba
na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Jakaya Mrisho Kikwete, walionyesha
kuguswa na msiba huo mzito.
Kabla
ya kifo chake, marehemu Sajuki, aliugua kwa miaka miwili, hali iliyosababisha
aende India kutibiwa, ambapo safari hiyo ilitokana na michango ya Watanzania
wenye mapenzi na kijana huyo.
Hata
hivyo, safari ya Sajuki ilizua ugonjwa mwingine katika uchunguzi wa madaktari
ambao kwa pamoja walisema msanii huyo alikuwa na ugonjwa kansa ya ngozi.
Mara
baada ya kurudi jijini Dar es Salaam, msanii huyo alikuwa kwenye afya kwa kiasi
kidogo, hata hivyo changamoto za kupata fedha za kumrudisha tena nchini India
Desemba mwaka jana, zilimfanya Sajuki ashindwe kurudi huko, licha ya kuhangaika
kwa kiasi kikubwa, ikiwamo kufanya shoo mbalimbali.
Mwaka
jana mwishoni, Sajuki alifanya shoo jijini Arusha, ambapo matokeo yake yalikuwa
machungu zaidi baada ya msanii huyo kuanguka na kuwahishwa hospitali ya Amana,
alipomzishwa kwa muda na baadaye kupelekwa Muhimbili alipoiaga Dunia na kuacha majonzi kwa Watanzania wapenda sanaa za maigizo na filamu hapa nchini.
No comments:
Post a Comment