https://tpc.googlesyndication.com/simgad/8045142562622600543


Recent Post

Saturday, January 13, 2018

Watanzania wanaoishi Saudi Arabia washerehekea Sikukuu ya Mapinduzi Riyadh Palace Hotel na Balozi Mgaza

Baadhi ya Watanzania wakiwa katika picha ya pamoja na Balozi Mgaza katikati mwenye suti.

Na mwandishi maalum, Riyadh - Saudi Arabia
Wanadiaspora na Watanzania waishio Riyadh nchini Saudi Arabia walisherehekea na kuandhimisha miaka 54 ya Mapinduzi ya Zanzibar  siku ya ijumaa tarehe 12 Januari, 2018 katika ukumbi wa Riyadh Palace Hotel. 

Sherehe hizo zilindaliwa na jumuiya ya Watanzania 'Tanzania Walfare Society' ambapo waalikwa mbalimbali kutoka miji ya Riyadh, Qasim na maeneo ya karibu walihudhuria. Mgeni rasmi katika sherehe hiyo alikuwa Balozi wa Tanzania nchini Saudi Arabia, Mhe. 

Hemedi Mgaza. Miongoni mwa walihudhuria sherehe hizo pia walikuwa wanafunzi wa vyuo vikuu, wafanyakazi wapya wa kampuni ya ufugaji ng'ombe wa Maziwa ya Al Marai na wengine kutoka kampuni ya ufugaji kuku ya Al Watania.  Kwa picha na habari zaidi angalia kupitia you tube 'Prince eddycool'
Mwenyekiti wa Jumuiya ya Watanzania ya Riyadh, Bw. Fuad Mabruk akitoa hotuba mbele ya Watanzania na wanadiaspora wa mji wa Riyadh huku nyuma yake walioketi kwenye meza kuu kuanzia kulia ni Makamu wa Mwenyekiti wa Jumuiya Dkt. Mahmoud Tuli, Balozi wa Tanzania nchini Saudi Arabia Mhe. Hemedi Mgaza, Afisa Mkuu wa Utawala wa Ubalozi Bw. Ahmada Sufiani, Katibu wa Jumuiya ya Watanzania Bw. Saeed Al Jabry na wa kwanza kushoto ni Mweka Hazina wa Jumuiya Bw. Mohamed Saeed.
 Balozi wa Tanzania nchini Saudi Arabia, H.E Hemed Mgaza, akizungumza na Watanzania.
Baadhi ya Watanzania na wanadiaspora wakisikiliza hotuba zilizokuwa zikitolewa na baadaye walipata fursa ya kuuliza maswali na kutoa maoni.

No comments:

LinkWithin

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...