Na Mwandishi Wetu, Handeni
WADAU wa mambo ya utamaduni yakiwamo mashirika, makampuni na
watu mbalimbali wameombwa kujitokeza kuliwezesha tamasha la Handeni Kwetu 2014,
lililopangwa kufanyika Desemba 13 mwaka huu wilayani Handeni, mkoani Tanga.
Mratibu Mkuu wa Tamasha la Handeni Kwetu, Kambi Mbwana, pichani.
Tamasha hilo linafanyika huku mwaka jana likiwezeshwa kwa
kiasi kikubwa na Shirika la Mfuko wa Hifadhi ya Jamii (NSSF) kwa ushirikiano na
wadau mbalimbali walioliwezesha tamasha hilo kwa mara ya kwanza katika Historia
ya Mkoa wa Tanga.
Akizungumza mjini hapa, Mratibu Mkuu wa Tamasha hilo, Kambi
Mbwana, alisema kuwa wadhamini wakijitokeza kwa wingi kutaongeza chachu ya
maendeleo ya nchi, sanjari na sanaa ya utamaduni inayotakiwa kuungwa mkono na
watu wengi.
Alisema kuwa kitendo cha wadhamini kuendelea kuliunga mkono
Tamasha hilo kutachangia kwa kiasi kikubwa kuinua uchumi wa nchi pamoja na
kutangaza utamaduni wa Mtanzania.
“Mwaka jana wadau wengi walijitokeza kuliwezesha tamasha la
Handeni, wakiwamo NSSF, hivyo tunaomba msimu huu pia tuendelee kushirikiana
kuliwezesha Tamasha la Handeni Kwetu litakalofanyika Desemba 13 mwaka huu,
Handeni Mjini.
“Hadi wakati
huu, walioonyesha nia ya kulisaidia tamasha la Handeni Kwetu 2014 ni pamoja na SmartMind & Partners iliyopo
chini ya Anesa Co. Ltd kwa kupitia kitabu chao cha Ni Wakati wako wa Kung’aa,
Phed Trans, chini ya Yusuphed Mhandeni, Handeni Kwetu Foundation, Wait &
Watch Film Company Ltd, Qs Mhonda J Apex Group of Companies Ltd na Skyblue
Security and Risk Mgt Ltd,” alisema Mbwana.
Tamasha la Handeni Kwetu ni miongoni mwa matukio makubwa ya
kiburudani mkoani Tanga, ambako zaidi ya watu 500 walihudhuria tamasha hilo
ambalo kwa mwaka huu mipango kabambe ya kuhakikisha kuwa linafanyika kwa
mafanikio.
No comments:
Post a Comment