NaKambi Mbwana, Dar es Salaam
TIMU ya Yanga, imeitangazia hali ya hatari Mgambo JKT,
ikisema itahakikisha inaibuka na ushindi mnono katika mchezo huo uliopangwa
kufanyika Jumanne ya Oktoba 29 katika Uwanja wa Taifa, jijini Dar es Salaam.
Kocha msaidizi wa Yanga, Fredy Minziro.
Mechio hiyo inachezwa huku Yanga wakiwa na shauku ya kuibuka
na ushindi huo ili iweze kujiweka pazuri katika patashika ya Ligi ya Tanzania
Bara, ambapo katika mechi iliyopita, mabingwa hao watetezi waliibuka na ushindi
wa bao 3-0 dhidi ya Rhino Rangers ya mjini Tabora.
Akizungumza jana jijini Dar es Salaam, Kocha Msaidizi wa
timu hiyo, Fredy Minziro, alisema kwamba timu yao imeanza mazoezi kwa ajili ya
kujiwinda na Mgambo huku wakiwa na hamu ya kushinda dhidi ya Mgambo JKT.
Alisema kuwa kikosi chao chote kimeanza mazoezi makali kwa
ajili ya mechi hiyo itakayokuwa na ushindani wa aina yake, kutokana na timu
zote mbili kutaka kushinda dhidi ya
mwenzake, jambo ambalo kwa upande wa Yanga wanakabiliana nalo.
“Tumekusudia kushinda mechi tatu mfululizo ili tupate pointi
28 ambazo tunaamini tutakuwa tumemalizia mzunguuko wa kwanza wa ligi kw3a kuwa
kileleni, hivyo lazima tufanikishee katika hilo ili tutimize kiu yetu.
“Ingawa tunajua mchezo huu utakuwa mgumu kupita kiasi, ila
hatuna sababu ya kushindwa kufanya vyema kwakuwa lengo letu ni kutetea ubingwa
wetu na lazima tuupate kwa kuhakikisha kuwa tunakuwa kitu kimoja na tunashinda
kila mechi,” alisema.
Kwa mujibu wa Minziro, kikosi chao kinaendelea na mazoezi
katika Uwanja wa Shule ya Sekondari Luyola, ambapo lengo lao ni kuibuka na
ushindi mnono katika mechi hiyo dhidi ya Mgambo JKT, Jumanne ijayo.
No comments:
Post a Comment