Na Kambi Mbwana, Dar es Salaam
KOCHA msaidizi wa klabu ya Yanga, Fredy Minziro, amesema
wameweka kando matokeo ya sare ya mabao 3-3 dhidi ya watani zao Simba, badala
yake wanaangalia mechi ijayo dhidi ya Rhino Rangers ya mjini Tabora, mechi
itakayopigwa kesho Jumatano katika Uwanja wa Taifa, jijini Dar es Salaam.
Kocha msaidizi wa timu ya Yanga, Fred Minziro, pichani.
Katika mechi ya watani wa jadi, Yanga walishinda bao 3 katika kipindi cha kwanza, wakati Simba wao walifanikiwa kusawazisha bao zote katika kipindi cha pili cha mchezo huo.
Katika mechi ya watani wa jadi, Yanga walishinda bao 3 katika kipindi cha kwanza, wakati Simba wao walifanikiwa kusawazisha bao zote katika kipindi cha pili cha mchezo huo.
Akizungumza jana jijini Dar es Salaam, Minziro alisema ni
ngumu kutamka kuwa kuna hujuma ndani ya kikosi chao, badala yake wote wageukie
mchezo ujao wa ligi dhidi ya Rhino.
Alisema japo wanachama na mashabiki wa Yanga wameumia, lakini
kwakuwa lengo lao ni kutetea ubingwa wao, ni jukumu la kila mmoja kuweka mipango
yake kwa ajili ya kuona timu yao inaibuka na ushindi mnono katika mchezo ujao.
“Ile ilikuwa mechi ngumu na wachezaji wetu hawakuwa makini
katika kipindi cha pili kiasi cha kuwafanya Simba wapate droo katika mchezo ambao
kila mmoja alijua tunatoka na ushindi mnono.
“Wote tuliumia katika matokeo yale, lakini kwakuwa lengo letu
ni ubingwa, nadhani huu ni wakati wa kila mmoja wetu kushikana kwa nia ya
kuhakikisha mambo yanakuwa mazuri,” alisema Minziro.
Yanga jana iliendelea na mazoezi yake katika Uwanja wa
Loyola, jijini Dar es Salaam, huku wachezaji wakijifua kwa ajili ya kuhakikisha
kuwa wanaibuka na ushindi dhidi ya Rhino Rangers.
Awali, Msemaji wa Yanga, Baraka Kizuguto, aliwataka wadau wa
Yanga na wanachama kwa ujumla, kuacha kusikiliza fitina zinazoweza kuanzishwa
kutokana na matokeo hayo.
“Mpira una matokeo ya kushangaza mno, ila hakuna sababu ya
kuanza kujadili mchezo huo zaidi ya kuangalia namna gani kikosi chao kitaibuka
na ushindi katika michezo inayofuata,” alisema.
Matokeo ya mabao 3-3 yalipokewa kwa furaha kwa upande wa
Simba, huku Yanga wao wakiondoka kichwa chini kutokana na kushindwa kulinda
mabao yao katika mchezo huo.
No comments:
Post a Comment