Na Kambi Mbwana, Dar es Salaam
Jamal Emil Malinzi ndiye Rais mpya
wa Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF), huku akishinda wadhifa huo
katika uchaguzi uliofanyika jana jijini Dar es Salaam.
Rais wa Shirikisho la Soka nchini TFF, Jamal Malinzi.
Aliibuka na ushindi wa kura 73 dhidi
ya mpinzani wake pekee Athuman Jumanne Nyamlani aliyepata kura 52. Nafasi ya
Makamu wa Rais imetwaliwa na Wallace Peter Karia aliyepata kura 67 na
kuwashinda Ramadhan Omari Nassib kura 52 huku Imani Omari Madega akipata kura
sita.
Akizungumza mara baada ya
kuchaguliwa, Rais Malinzi ametaka ushirikiano kutoka kwa wadau wote akiwemo
mpinzani wake Nyamlani katika kuhakikisha mpira wa miguu nchini unasonga mbele.
Pia ametoa msamaha kwa watu wote
waliokuwa wamefungiwa kuanzia ngazi ya wilaya, mkoa na TFF. Msamaha huo
hauwahusu wale waliofungiwa kwa makosa ya rushwa au kupanga matokeo. Vilevile
msamaha huo hauhusu adhabu zilizotolewa katika ngazi ya klabu.
Rais Malinzi pia amevunja kamati
zote za TFF ambapo ataziunda upya kwa kushirikiana na Kamati ya Utendaji.
Kwa upande wa wajumbe wa Kamati ya
Utendaji walioshinda ni Kalilo Samson (Kanda namba 1- Geita na Kagera)
aliyepata kura 102 za ndiyo na 17 za hapana. Kanda namba 2- Mara na Mwanza,
mshindi ni Vedastus Lufano aliyepata kura 51 dhidi ya Jumbe Odessa Magati (11),
Mugisha Galibona (24), na Samwel Nyalla (39).
Epaphra Swai ndiye mshindi wa Kanda
namba 3- Shinyanga na Simiyu kwa kura 63 dhidi ya Mbasha Matutu aliyepata 61.
Kanda namba 4- Arusha na Manyara mshindi ni Omali Walii Ali aliyepata
kura 53 dhidi Elley Mbise (51), Ally Mtumwa (19).
Kanda namba 4- Kigoma na Tabora,
mshindi ni Ahmed Idd Mgoyi aliyepata kura 92 dhidi ya 28 za Hamisi Yusuf
Kitumbo.
Ayubu Nyaulingo na Blassy Mghube
Kiondo ameshinda Kanda namba 6- Katavi na Rukwa kwa kura 73 dhidi ya Ayubu
Nyaulingo aliyepata 52. Ayoub Shaibu Nyenzi ndiye mshindi wa Kanda namba 7-
Iringa na Mbeya kwa kupata kura 59 na kuwapiku David Samson Lugenge (8), John
Exavery Kiteve (12) na Lusekelo Elias Mwanjala (46).
Kanda namba 8- Njombe na Ruvuma
inawakilishwa na James Patrick Mhagama aliyepata kura 93 dhidi ya 31 za Kapteni
mstaafu Stanley William Lugenge. Athuman Kingombe Kambi ndiye mshindi wa Kanda
namba 9- Lindi na Mtwara kwa kura 84 akiwazidi Francis Kumba Ndulane (30) na
Zafarani Mzee Damoder (11).
Hussein Zuberi Mwamba ametetea
ujumbe wa Kanda namba 10- Dodoma na Singida kwa kura 63 akiwapiku Stewart
Masima (58) na Charles Komba (4). Geofrey Irick Nyange ameshinda Kanda namba
11- Morogoro na Pwani akipata kura 78 dhidi ya Juma Pinto (26), Farid Nahdi
(14), Riziki Juma Majala (5) na Twahil Twaha Njoki (2).
Kanda namba 12- Kilimanjaro na
Pwani, Khalid Abdallah Mohamed ndiye aliyeibuka kidedea kwa kura 69 dhidi ya 54
za mpinzani wake Davis Elisa Mosha. Kidao Wilfred Mzigama ameshinda Kanda
namba 13- Dar es Salaam kwa kupata kura 60 dhidi ya wapinzani wake Muhsin Said
Balhabou (50), Omar Isack Abdulkadir (10) na Alex Crispine Kamuzelya (4).
No comments:
Post a Comment