Na Kambi Mbwana, Dar es Salaam
MECHI ya watani wa jadi wa Simba na
Yanga, inapigwa leo katika Uwanja wa Taifa, jijini Dar es Salaam, huku kila
mmoja ikijigamba kuweza kuibuka na ushindi mnono.
Kocha msaidizi Jamhuli Kihwelo Julio akiongoza kikosi chake katika mazoezi ya timu ya Simba. Picha na maktaba yetu.
Mechi hiyo inapigwa wakati Yanga wanaingia uwanjani wakitokea Pemba, mjini Zanzibar, huku Simba wao wakiwa wameweka kambi yao Bamba Beach, Kigamboni.
Mechi hiyo inapigwa wakati Yanga wanaingia uwanjani wakitokea Pemba, mjini Zanzibar, huku Simba wao wakiwa wameweka kambi yao Bamba Beach, Kigamboni.
Katika mchezo huo unaosubiriwa kwa
hamu na mashabiki wa soka Tanzania na Barani Afrika kwa ujumla, Simba wapo
mbele kwa pointi 18 dhidi ya Yanga yenye pointi 18.
Kelvin Yondan, ana kazi kubwa leo uwanjani kuhakikisha kuwa timu yake haifungwi na Simba katika Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam leo jioni.
Endapo Simba itashinda mbele ya Yanga, basi itazidi kujikita kileleni kwa kujikusanyia jumla ya pointi 21 na kumuacha mtani wake wa jadi, ambaye ndio Bingwa mtetezi.
Endapo Simba itashinda mbele ya Yanga, basi itazidi kujikita kileleni kwa kujikusanyia jumla ya pointi 21 na kumuacha mtani wake wa jadi, ambaye ndio Bingwa mtetezi.
Kwa kulijua hilo, Yanga wao
wamepania zaidi waibuke na ushindi kwa ajili ya kumkuta mtani wake yenye pointi
hizo 18, hivyo endapo itafanikiwa, watafungana pointi na kuangalia idadi ya
magoli ya kufungwa na kushinda.
Hata hivyo, katika mechi hiyo Simba
wameweka umakini wa hali ya juu, kiasi cha kuwa kimya hata kwenye vyombo vya
habari tofauti na wenzao Yanga wanaojitapa.
Mara kadhaa kwa kupitia viongozi
wao, Yanga imetangaza kadhia ya mabao kwa mtani wao, huku Katibu wa Baraza la
Wazee, Ibrahim Akilimali akitangaza ushindi wa mabao 3-0 kwa mara tano
mfululizo na kuwapa imani kubwa wanachama na mashabiki wao.
Shirikisho la Soka nchini (TFF), juzi
lilitangaza viingilio vya mechi hiyo, huku kiingilio cha chini kabisa kuwa Sh.5,000,
ikifuatiwa na viti vya rangi ya bluu ambavyo viingilio vyao ni sh. 7,000.
Viingilio vingine ni viti vya rangi
ya chungwa sh. 10,000, VIP C ni sh. 15,000, VIP B sh. 20,000 wakati VIP A ni sh.
30,000.
Kwa kawaida, mechi ya Simba na Yanga
imekuwa na shangwe za kila aina kutoka kwa mashabiki wao waliotapakaa nchi
nzima, ambapo kila mmoja ana hamu ya kuona anatoka akiwa mwenye furaha.
Ofisa Habari wa Simba, Ezekiel
Kamwaga, ambaye ndio mzungumzaji mkubwa katika klabu hiyo, alisema kuwa timu
yao ipo katika kiwango kizuri kwa ajili ya kumenyana na mtani wao.
“Hakuna haja ya kushikwa na woga juu
ya mechi hii kwasababu wachezaji wetu wapo imara kwa ajili ya kushinda na kukaa
kileleni kwa pointi 21 ambazo ni muhimu mno kwetu, hivyo mashabiki waje kwa
wingi kuona ushindi,” alisema.
Naye Kocha Msaidizi wa Yanga, Fredy
Minziro, aliwapongeza wadau na wazee wa klabu yao Kisiwani Pemba kwa kuwapokea
vizuri na kuwapa Baraka zote kwa ajili ya kuhakikisha kuwa wanaibuka na ushindi
mnono dhidi ya Simba.
Simba kutoka na ushindi dhidi ya
Yanga ni jambo lisilowezekana hata kidogo, hivyo tupo tayari kwa kuwaonyesha
uwezo wa soka uwanjani na hakika kazi watakuwa nayo hiyo kesho (leo),” alisema
Minziro.
Mechi
hiyo namba 63 itachezeshwa na Israel Nkongo kutoka Dar es Salaam, huku
akisaidiwa na Hamis Changwalu wa Dar es Salaam na Ferdinand Chacha wa Bukoba, bila
kusahau Oden Mbaga wa Dar es Salaam, akiwa ni mwamuzi wa akiba.
Kwa mujibu wa taarifa za mchezo huo
kutoka ofisi za TFF, Kamishna wa mechi hiyo atakuwa John Kiteve kutoka Iringa
wakati mtathmini wa waamuzi (referees assessor) ni Stanley Lugenge wa Njombe.
No comments:
Post a Comment