Balozi
wa kudumu wa African Union Mhe. Amina Salum Ali akiwashukuru wageni
waalikwa wakiwiwemo Waheshimiwa Mabalozi kutoka nchi mbalimbali kutoka
bara la Afrika wanaowakilisha nchi zao nchini Marekani kwa kufika kwao
kwenye chakula cha jioni Fairmont Hotel iliyopo Washington, DC
walichomuandalia mwanamuziki maarufu kutoka Afrika ya Kusini, Yvonne
Chaka Chaka kwa heshima ya kuwa Balozi wa kampeni ya kutokomeza ugonjwa
wa malaria Barani Afrika. Balozi Amina Salum Ali aliwashukuru Benki ya
Dunia kwa juhudi za makusudi wanazofanya kuhakikisha Bara la Afrika
linatokomeza kabisa gonjwa hili hatari la Malaria, pia Balozi Amina
Salum Ali alimshukuru Bwn. Tim Ziemer kutoka USAID kwa jitihada zao za
kupigana kuutokomeza ugonjwa wa malaria Duniani hususani Bara la Afrika.
Kushoto
ni Mwanamuziki wa Afrika ya Kusini Yvonne Chaka Chaka akifuatilia
hotuba ya Balozi wa African Union Mhe. Amina Salum Ali, kulia ni Kaimu
Balozi wa Afrika ya Kusini nchini Marekani Mhe. Johnny Moloto.
Kutoka
kushoto ni Mhe. Balozi wa Swaziland Rev. Dr. A. M. Ntshangase, Balozi
wa Tanzania nchini Marekani Mhe. Liberata Mulamula na Balozi wa Botswana
nchi Marekani Mhe. Dr.Tebelelo Mazile Seretse.
Dr.
Anne Maryse B. Pierre-Louis ambaye ni mkuu wa utawala na mtaalam wa
maswala ya afya kutoka Benki ya Dunia akielezea jitihada za Benki ya
Dunia inazofanya kupigana kuutokomeza ugonjwa wa Malaria Barani Afrika.
Pia alimshukuru mwanamuziki kutoka Afrika ya Kusini, Yvonne Chaka Chaka
kwa kazi nzuri anayofanya ya kuwa Balozi wa kampeni ya kutokomeza
ugonjwa wa Malaria Barani Afrika.
Dr. Anne Maryse B. Pierre-Louis akimpa mwanamuziki Yvonne Chak Chaka zawadi ya maua ambayo yametoka Afrika ya Kusini.
Mwanamuziki
Yvonne Chaka Chaka akimshukuru Balozi Amina Salum Ali na African Union
kwa kumuandalia chakula cha usiku maalum kwa kutambua mchango wake wa
kampeni ya kupigana na kuwaelimisha hasa wakina mama na watoto wa Afrika
ambao ndio waathirika namba moja na gojwa hili la malaria na akaelezea
sababu ya yeye kuamua kuwa Balozi wa kampeni hii ni siku mmoja wa
wanamuziki wake alipokufa kutokana na malaria ndipo aliguswa na kuamua
kuwaelimisha wanawake wenzake hususai waishio vijijini na kazi hiyo
ameifanya ipasavyo kwani mpaka hapo anapoongea ameishatembelea nchi zote
za Afrika mijini mpaka vijijini kuelimisha na hatimae kuutokomeza
ugonjwa huu wa malaria barani Afrika.
Tim
Ziemer kutoka USAID akielezea jitihada wanazofanya kwenye kampeni ya
kuutokomeza Malaria Duniani Bara la Afrika likiwa limepewa kipaumbele.
Mhe.
Liberata Mulamula akichangia hoja ya malaria kwa kuelezea jitihada za
Tanzania akiwemo Rais Jakaya Kikwete za kupigana mpaka mwisho na
kuhakikisha malaria Tanzania inatokomezwa kabisa pia Balozi Mulamula
aliezea jitihada zilizofanywa na serikali ya kuutokomeza malaria
Zanzibar lakini changamoto kubwa Serikali inayokabiliana nayo ni
Tanzania Bara ambako malaria bado ipo.
Kutoka
kushoto ni Dr. Anne Maryse B. Pierre-Louis wa Benki ya Dunia, Mhe.
Balozi wa Rwanda nchini Marekani Prof. Mathilde Mukantabana, mwanamuziki
toka Afrika ya Kusini Yvonne Chaka Chaka, Balozi wa Tanzania nchini
Marekani Mhe. Liberata Mulamula na Balozi wa African Union nchini
Marekani Mhe. Amina Salum Ali katika picha ya pamoja.
Juu na
chini ni Mabalozi kutoka nchi za Afrika wanaowakilisha nchi zao nchini
Marekani, Balozi wa African Union na mwanamuziki kutoka Afrika ya Kusini
Yvonne Chaka Chaka katika picha ya pamoja.
Mabalozi
kutoka nchi za Afrika wanaowakilisha nchi zao nchini Marekani, Balozi
wa African Union na mwanamuziki kutoka Afrika ya Kusini Yvonne Chaka
Chaka wakiwa kwenye meza ya chakula picha na Vijimambo Blog
No comments:
Post a Comment