Na Kambi Mbwana, Dar es Salaam
MECHI ya kusisimua kati ya
Nkhwamba na Azam zinazoshiriki Kombe la Kata ya Mrijo, iliyopo wilayani Kondoa
mkoani Dodoma, itanarajiwa kupigwa kesho katika Uwanja wa Shule ya Msingi Mrijo
wilayani humo.
Mechi hiyo ni marudio baada ya
ule uliochzewa Alhamis iliyopita kumalizika kwa daakika 90 huku zikifungana bao
1-1 hivyo kuamuriwa kuongezwa dakika nyingine 30, ambapo hata hivyo hazikuchezwa
kutokana na giza kuingia, hivyo kuahirishwa hadi kesho Jumatano.
Akizungumza kwa njia ya simu
akitokea wilayani Kondoa, moja ya wawezeshaji wa timu ya Azam yenye
kushirikisha vijana wenye umri mdogo, Rashid Dogodogo, alisema kwamba
mashindano hayo yamekuwa na mvuto wa aina yake katika Kata hiyo wilayani Kondoa
mkoani Dodoma.
Alisema mechi hiyo ni hatua ya
robo fainali, huku mashindano hayo yakishirikisha timu mbalimbali zenye uwezo
wa juu wa kucheza soka na kufurahisha wadau wengi wa mpira wa miguu wilayani
humo.
“Mchezo huu utachezwa kwa dakika
zote 90 baada ya juzi kushindwa kupatikana mshindi, hivyo ni matumaini yetu
kuwa mchezo huu utakuwa wa aina yake na kufurahisha watu wengi.
“Mbali na mechi ya Azam na
Nkhwamba itakayochezwa Jumatano, pia
Ijumaa iliyopita kulikuwa na mchezo wa kusisimua kati ya Kimetro na Kambugwe, huku
Kambugwe ilikifanikiwa kutoka na ushindi wa mabao 3-2 dhidi ya Nkhwamba,”
alisema.
Timu ya Azam inafadhiliwa na
Khadija Rashid, Khamis Msakati na Dogodogo, wakati wafadhili wa Kimetro ni
Hassan Choma na Omari Kipara, huku kocha wa Nkhwamba akiwa ni Shaban Juma Baba,
wakati ile ya Azam inanolewa na Hamza Ramadhan na kocha wa Kimetro ni Kaifa
Nduko.
Baadhi ya timu nyingine
zinazoshiriki mashindano hayo ni Ndido, Njolo, Wakata Miwa, Mapango na
nyinginezo zinazoshiriki patashika hiyo ya Kombe la Kata ya Mrijo, wilayani
Kondoa mkoani Dodoma.
No comments:
Post a Comment