Na Kambi Mbwana, Dar es Salaam
MWANDISHI wa ITV na Radio One, Ufuo Saro amepigwa amepigwa
risasi ya tumbo na kwenye paja na sasa yupo katika Hospitali ya Taifa Muhimbili
akiendelea na matibabu huku hali yake ikiwa si ya kuridhisha.
Mwandishi wa ITV na Radio One, Ufoo Saro, pichani, aliyepigwa risasi, ambapo mama yake amefariki Dunia katika tukio hilo.
Katika tukio hilo, mama yake mzazi Saro, anayejulikana kwa
jina la Anastazia Peter Saro naye alipigwa risasi ya kwenye matiti na kupelekea
kifo chake papo hapo, katika tukio linalodaiwa kufanywa na na mtu anayejulikana
kwa jina la Mushi ambaye pia alifariki kwa kujipiga risasi.
Kamanda wa Polisi mkoa wa Kipolisi Kinondoni, Camilius
Wambura, aliuambia mtandao wetu wa Handeni Kwetu kuwa, kuwa uchunguzi wa awali unaendelea, huku Ufoo Saro mwenyewe
akishindwa kuzungumzia suala kwakuwa yupo chini ya uangalizi ya
madaktari Muhimbili.
Mushi anayefanya kazi UN nchini Sudan, aliwasili jana
akitokea eneo lake la kazi ambapo enzi za uhai wake alizaa na Saro. Kamanda
huyo anaendelea kusema kuwa, Mushi alifikia eneo la Mbezi Magari Saba, jijini
Dar es Salaam, kabla ya leo saa 12:30 kufika kwa mkwe wake nyumbani kwa kina
Saro.
Baada ya kufika hapo, alitoa bastola yake na kumpiga mkwe
wake, mzazi mwenzake na kujimaliza mwenyewe, ambapo bado uchunguzi unaendelea
kujua kiini cha sakata hilo.
“Taarifa hizi zitakamilika pale Ufo Saro atakapohojiwa na
polisi kwakuwa yeye ndio mhusika kwakuwa nyumba ile ilikuwa na watu watatu,
ambapo wawili kati yao ni marehemu.
“Tutaendelea kulifanyia kazi suala hili, ambapo sasa
majeruhi yupo Muhimbili akipatiwa matibabu wakati miili ya marehemu pia
imehifadhiwa katika chumba cha kuhifadhia maiti katika Hospitali hiyo ya Taifa,
Muhimbi,” alisema.
Watu mbalimbali katika mitandao ya kijamii wameonyesha
kushangazwa na tukio hilo alilofanyiwa mwanadada huyo anayefanya kazi katika
kituo cha ITV na Radio One, kinachomilikiwa na Kampuni ya IPP, chini ya
Mwenyekiti wake Reginald Mengi.
No comments:
Post a Comment