Na Kambi Mbwana, Dar es Salaam
Mechi
ya Ligi Kuu ya Vodacom (VPL) kati ya wenyeji Simba na Tanzania Prisons
kutoka Mbeya iliyochezwa jana (Oktoba 12 mwaka huu) Uwanja wa Taifa, Dar
es Salaam imeingiza sh. 60,521,000.
Msemaji wa TFF, Boniface Wambura, pichani.
Simba
iliibuka na ushindi wa bao 1-0 katika mechi hiyo namba 55 na
kushuhudiwa na watazamaji 10,494 waliokata tiketi kwa viingilio vya sh.
5,000, sh. 8,000, sh. 15,000 na sh. 20,000.
Msemaji wa Shirikisho la Soka nchini TFF, Boniface Wambura, alisema kuwa kila klabu ilipata mgawo wa sh. 14,191,002.55 wakati Kodi ya Ongezeko la Thamani (VAT) iliyolipwa ni sh. 9,232,016.95.
Mgawo
mwingine wa mapato hayo ni asilimia 15 ya uwanja sh. 7,215,763.96,
tiketi sh. 3,183,890, gharama za mechi sh. 4,329,458.37, Kamati ya Ligi
sh. 4,329,458.37, Mfuko wa Maendeleo ya Mpira wa Miguu (FDF) sh.
2,164,729.19 na Chama cha Mpira wa Miguu Mkoa wa Dar es Salaam (DRFA)
sh. 1,683,678.26.
No comments:
Post a Comment