Na Kambi Mbwana, Dar es
Salaam
MWIMBAJI wa muziki wa kizazi kipya,
Pili Juma, maarufu kama Vida, amesema malengo yake ni kufanya kazi nzuri kwa
ajili ya kuonyesha kipaji chake katika kona ya muziki wa kizazi kipya nchini.
Vida akiwa kwenye pozi.
Vida anayetamba na wimbo
wake wa Baba Awena, huku akimshirikisha nyota wa muziki nchini, Linex, anatokea
katika taasisi ya kukuza na kulea vipaji ya Tanzania House of Talent THT.
Akizungumza jana jijini
Dar es Salaam, Vida alisema kuwa sanaa ya muziki kwake ni kipaji, hivyo
anaamini malengo yake yatatimia kwa kuweka mkazo kwenye utendaji wake wa kazi.
Alisema kuwa japo anajua
changamoto na ugumu uliopo katika tasnia hiyo, ila amejipanga vizuri kwa ajili
ya kutimiza malengo yake katika tasnia ya muziki huo nchini.
“Nimekuwa nikifanya juhudi
kubwa kuhakikisha kuwa mambo yangu yanakuwa mazuri pamoja na kuwapa burudani
kamili wadau na mashabiki wa muziki wa kizazi kipya hapa nchini.
“Najua ugumu uliopo
lakini si sababu ya kunifanya nishindwe kuongeza bidii na kukuza harakati zangu
katika tasnia hiyo, ukizingatia kuwa ndio malengo yangu ya kutangaza muziki
huu,” alisema Vida.
Vida ni miongoni mwa
wasanii mahiri wa kike wanaotokea katika taasisi hiyo ya THT yenye vichwa
kadhaa, akiwamo Recho, Mwasiti, Linah na wengineo wanaofanya vizuri katika
muziki huo.
No comments:
Post a Comment