Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mbeya, Athumani Diwani, pichani.
Wilaya ya Mbeya Mjini – kupatikana na miche ya
bangi.
Mnamo tarehe 06.10.2013 majira ya saa 14:00hrs
huko eneo la Uyole jiji na mkoa wa Mbeya, askari polisi wakiwa doria walimkamata
Julius s/o Mwambenje, miaka 23, kyusa, mkulima, mkazi wa Nsalaga, Uyole akiwa
na bangi misokoto 15 sawa na uzito wa gram 75.
Mbinu ni kuficha bangi hiyo kwenye mfuko wa
rambo. mtuhumiwa ni mvutaji wa bangi. taratibu zinafanywa ili afikishwe
mahakamani. kamanda wa polisi mkoa wa mbeya kamishna msaidizi wa polisi diwani
athumani anaendelea kutoa wito kwa jamii kuacha matumizi ya dawa za kulevya
kwani ni kinyume cha sheria na ni hatari kwa afya ya mtumiaji.
Wilaya ya Mbeya Mjini – kuingia nchini bila
kibali
Mnamo tarehe 06.10.2013 majira ya saa 23:30hrs
huko eneo la stendi kuu jiji na mkoa wa mbeya. askari polisi wakiwa doria
walimkamata 1. nyelakozi d/o melania, miaka 33, mkulima, na 2. ndaishimili d/o
teonya,miaka 33,wote raia na wakazi wa nchini burundi wakiwa na watoto 11 ambao
pia ni raia wa burundi wakiwa wameingia nchini bila kibali.
Mbinu ni kusafiri kwa njia ya kificho.
taratibu zinafanywa ili wakabidhiwe idara ya uhamiaji. Kamanda wa polisi mkoa
wa mbeya kamishna msaidizi wa polisi diwani athumani anatoa wito kwa jamii
kuendelea kutoa taarifa katika mamlaka husika juu ya mtu/watu wanaowatilia
shaka ikiwa ni pamoja na wahamiaji haramu ili hatua za kisheria zichukuliwe
dhidi yao.
Wilaya ya Chunya – kupatikana na pombe haramu
ya moshi gongo.
Mnamo tarehe 06.10.2013 majira ya saa 08:30hrs
huko katika kitongoji cha majengo kijiji cha lupa wilaya ya chunya mkoa wa
mbeya. askari polisi wakiwa doria walimkamata lyidia d/o ambakisye, miaka 25,
kyusa, mkulima, mkazi wa lupa akiwa na pombe haramu ya moshi[gongo] ujazo wa
lita 5.
Mtuhumiwa ni muuzaji wa pombe hiyo. taratibu
zinafanywa ili afikishwe mahakamani. kamanda wa polisi mkoa wa mbeya kamishna
msaidizi wa Polisi Diwani Athumani anaendelea kutoa wito kwa jamii kuacha
matumizi ya pombe haramu ya moshi [gongo] kwani ni kinyume cha sheria na ni
hatari kwa afya ya mtumiaji.
Wilaya ya Chunya – kupatikana na pombe haramu
ya moshi (gongo).
Mnamo tarehe 06.10.2013 majira ya saa 09:00hrs
huko katika kitongoji cha Magunga kijiji cha Mamba wilaya ya Chunya mkoa wa Mbeya,
askari polisi wakiwa doria walimkamata John s/o Lutimbo, miaka 29, msukuma,
mkulima, mkazi wa mamba akiwa na pombe haramu ya gongo ujazo wa lita 4.
Mtuhumiwa ni muuzaji wa pombe hiyo. taratibu
zinafanywa ili afikishwe mahakamani. Kamanda wa polisi mkoa wa mbeya kamishna
msaidizi wa polisi anatoa wito kwa jamii kuacha matumizi ya pombe haramu.
Diwani Athumani - ACP
Kamanda wa Polisi mkoa wa Mbeya
No comments:
Post a Comment