Na Kambi Mbwana, Dar es Salaam
WANACHAMA wa
Yanga wameombwa kujitokeza kwa wingi Makao Makuu ya klabu hiyo kuanzia leo
Oktoba 16 hadi Novemba 10 kwa ajili ya kupiga kura iwapo wanaafiki Yanga kuwa
Kampuni.
Mwenyekiti wa Yanga, Yusuf Manji, pichani.
Uamuzi huo
ulifikiwa katika Mkutano wa Kawaida wa Wanachama wa Yanga uliofanyika Januari 16
mwaka huu, huku Mwenyekiti kwa niaba ya Kamati ya Utendaji akiwapa Wanachama
wafikirie mapendekezo ya klabu yao kuwa Kampuni ama kutokuwa Kampuni kisha kuyawasilisha
kwa Katibu Mkuu wao.
Akizungumza
mapema leo asubuhi, Katibu Mkuu wa Yanga, Lawrence Mwalusako, aliwataka
wanachama wao kuchangamkia fursa hiyo ili suala hilo lifikie hatua nzuri.
“Nachukua
nafasi hii kuwaambia Wanachama wa Yanga kuwa kuanzia leo Oktoba 16 hadi Novemba
10 mwaka huu kuwa kutakuwa na sanduku moja (1) hapa klabuni kwa ajili ya kukusanya
kura za maoni ya Wanachama ya kuanzisha Kampuni (NDIYO) au kutokuwa Kampuni
(HAPANA)
“Kila
Mwanachama hai atakuwa na uhuru wa kupiga kura na atalazimika kuja na Kadi yake
ambapo itamzuia kupiga kura mara mbili au zaidi,” alisema Mwalusako.
Kwa mujibu wa
Mwalusako, zoezi hili ni muhimu kwa ajili ya maendeleo ya Yanga na kuwataka
wanachama wote wachangamkie fursa hiyo kwa ajili ya kupiga hatua baada ya
kutolewa wazo la Kampuni.
No comments:
Post a Comment