Na Kambi Mbwana, Dar es Salaam
KAMATI inayoandaa namna ya
kumuaga mwanamuziki mkongwe hapa nchini, Muhdini Gurumo, imesema inajipanga
upya baada ya kushindwa kufanya tamasha la Gurumo 55 juzi Oktoba 11 kama
walivyowatangazia Watanzania.
Mwenyekiti wa Kamati ya Gurumo 55 Asha Baraka akizungumza jambo kulia, akiafutiwa na Mzee Gurumo, Juma Mbizzo, Saidi Kibiriti katika moja ya matukio ya kutangaza tukio hilo ambalo kwa sasa limeota mbawa.
Akizungumza jana jijini Dar es Salaam, Mwenyekiti wa Kamati hiyo, ambaye pia ni Mkurugenzi wa bendi ya The African Stars Twanga Pepeta, Asha Baraka, alisema kuwa mchakato huo ulikabiliwa na matatizo mengi, yakiwakiwamo wadau wa kamati hiyo kubanwa na vitu vingine.
Akizungumza jana jijini Dar es Salaam, Mwenyekiti wa Kamati hiyo, ambaye pia ni Mkurugenzi wa bendi ya The African Stars Twanga Pepeta, Asha Baraka, alisema kuwa mchakato huo ulikabiliwa na matatizo mengi, yakiwakiwamo wadau wa kamati hiyo kubanwa na vitu vingine.
Alisema awali walipanga tamasha
la kwanza lifanyike Oktoba 11 mwaka huu katika Ukumbi wa Diamond Jubilee, ila
walishindwa kufanya hivyo kama walivyopanga.
Asha aliwatoa hofu Watanzania
na wadau wa muziki kuwa tukio hilo litafanyika kama ilivyopangwa, japo
haitakuwa kwa tarehe iliyowekwa hapo kabla.
“Katika matukio kama haya
kunahitaji mipango mingi, hivyo litafanyika kama ilivyopangwa na kuhakikisha
kuwa tunafanikisha dhamira zetu.
“Naamini siku chache zijazo
tutangaza upya namna gani tutafanya kwa ajili ya kumuaga mwanamuziki Gurumo na
kuweka mipango kabambe ya kuthamini mchango wake,” alisema Asha.
Kamati hiyo pia imekusanya watu
kadhaa, akiwamo Mkurugenzi wa Screen Masters Said Mdoe, Juma Mbizo na wengineo
waliokuwa na lengo moja la kufanikisha jambo hilo.
No comments:
Post a Comment