Naibu Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Ufundi, Phillip Mulugo, pichani.
Na Mwandishi Wetu, Dar es Salaam
SERIKALI kupitia Wizara ya Elimu na
Mafunzo ya Ufundi imekunjua makucha yake kwa kutangaza kuvifuta vyuo 10
ambavyo havikusajiliwa na Baraza la Taifa la Elimu ya Ufundi (NACTE) .
Naibu Waziri wa wizara hiyo, Philip Mulugo, alitoa kauli hiyo jijini Dar es Salaama mbele ya Kamati ya Bunge ya Huduma za Jamii na kuongeza kuwa kufutwa kwa vyuo hivyo ni kutokana na kutokufuata utaratibu wa kusajiliwa.
Alivitaja vyuo hivyo ni Media and Research Center, Vision Hotel and Tourism College, East Africa College of Hospitality and Tourism, The Africa Institute of Business Management na Aspiration Training Center, vyote vya Dar es Salaam.

Vingine ni Dar es Salaam School of
Hair Design, Media and Values Training Institute na Information
Technology Training Center vya Dar es Salaam. Pia alikitaja Chuo cha
Morogoro School of Medical Sciences cha Morogoro.
Katika hatua nyingine, Mulugo alikiri kuwa kuna upungufu katika kutoa mikopo kwa wanafunzi wa vyuo vikuu kupitia bodi ya mikopo.
Alisema kuna changamoto nyingi
zinazoikabili bodi hiyo zikiwamo urejeshwaji wa mikopo kwa wanafunzi
waliomaliza chuo, mfumo wa utoaji wa mikopo, ufinyu wa bajeti na makosa
yanayotokana na wanafunzi kukosea kujaza fomu za mikopo
No comments:
Post a Comment